Serikali imeendelea na msimamo wake wa kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, baada ya Rais Magufuli
kuondoa safari za nje, mamilioni ya pesa kuokolewa katika uzinduzi wa
Bunge sasa imepiga marufuku uchapishaji wa kadi za sikukuu ya
Christmas na mwaka mpya.
Katika taarifa yake Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Christmas na mwaka mpya kwa gharama za Serikali mwaka huu.
Balozi Sefue ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo afanye kwa gharama zake mwenyewe.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa
imesema fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji wa uchapishaji wa
kadi hizo zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, idara na Taasisi za
umma zinadaiwa na wananchi waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe
katika matumizi mengine.
Taarifa hiyo ilisomeka hivi
0 comments:
Post a Comment