MKUU
wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa amepiga marufuku uuzaji na unywaji wa
pombe wakati wa saa za kazi. Amri hiyo ameitoa jana katika taarifa yake
aliyoisambaza kwa vyombo vya habari.
Gallawa
alisema kwamba amechukua uamuzi huo kwa kuzingatia mamlaka aliyonayo
kwa mujibu wa Katiba, Ibara ya 61, Ibara ndogo ya 4.
Alisema kutokana na amri hiyo itakuwa marufuku kwa wakazi na wafanyabiashara wa mkoa huo kuuza au kunywa pombe kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni.
Alisema kutokana na amri hiyo itakuwa marufuku kwa wakazi na wafanyabiashara wa mkoa huo kuuza au kunywa pombe kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na nusu jioni.
0 comments:
Post a Comment