Wazee
wa kimila wa makabila ya Wakurya na Waluo wamesema watu watano
waliookolewa kutoka kwenye machimbo ya Nyangalata, Kahama ambao
waliwekewa matanga kabla ya kuibuka wanatakiwa kufanyiwa mambo ya
kimila, vinginevyo watakufa kiajabu.
Mmoja wa wazee hao, Ghati Ryoba (61) wa Mtaa wa Mwangaza, Nyamisangura – Tarime amesema: “Mtu
akidaiwa kuwa amekufa lakini baadaye akaonekana, wazee wa ukoo au wa
mila humfanyia matambiko kama njia ya kuondoa mikosi kwake na kwa
familia yake. Wanachukua kondoo mweusi wanamchinja kisha wanamtambikia
(bharamsendola).
“Kisha
wanachukua kinyesi cha kondoo (ubhuhu ghwaling’ondi) na mti mmoja
unaitwa (richirya) kisha kile kinyesi kinarushwarushwa ndani ya nyumba
yake na mji mzima kama kuna nyumba nyingine halafu wanachukua kile
kinyesi cha kondoo na kumpaka kwenye mikono na anashikana mikono na
watu.”
Mzee huyo wa kimila ameongeza kusema kuwa baada ya hapo atanawa mikono kabla ya kuruhusiwa kula na kujumuika na watu.
Amesema baada ya hapo atanyolewa kisha atakwenda kuoga “... Wengine hupeleka nywele kuzizindika kwenye mlima ambako watu hawalimi.”
Kuhusu Waluo, mzee Peter Odello wa Kitembe, Rorya amesema: “Kama
inatokea mtu anadaiwa kufa na watu wakafanya matanga lakini baadaye
akaonekana, lazima arudi kijijini wamfanyie matambiko.”
Amesema
akirudi, wazee watachinja ng’ombe na watu watakaa tena kama walivyokaa
kwenye matanga kwa siku mbili au tatu watu wakila kisha kupewa dawa
inayoitwa manyasi.
0 comments:
Post a Comment