Watu wawili mkoani Iringa wamefariki
dunia katika matukio mawili tofauti akiwemo kijana mmoja kuuwawa akiwa anaiba
spika ya redio.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
kamanda wa polisi mkoa wa iringa RPC RAMADHANI ATHUMANI MUNGI amesema kuwa
tukio hilo limetokea katika klabu cha pombe eneo la mpogole kata ya mkimbizi
mkoani hapa.
Katika tukio la pili kamanda MUNGI
amebainisha kuwa kumetokea ajali ya gari
katika eneo la RUNGREMBA njia kuu ya iringa mbeya na kusababisha kifo cha
EMRASI FRANK.
Wakati huohuo kamanda MUNGI ameongeza
kuwa jeshi la polisi linamshikilia PETER MPOGOLO kwa kosa kujichukulia sheria
mkononi na kuwataka wananchi kufuata sheria na si kumuua mtu.
0 comments:
Post a Comment