November 21 mechi za Ligi Kuu Uingereza zimeendelea tena baada ya kusimama kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali, klabu ya Chelsea inayofundishwa na kocha Jose Mourinho ilikuwa na kibarua kigumu cha kuanza kutafuta ushindi dhidi ya klabu ya Norwich City katika dimba lake la nyumbani Stamford Bridge.
Mechi hiyo ambayo kwa Chelsea ilikuwa ya 13 ya Ligi Kuu Uingereza
toka kuanza kwa msimu huu, ikiwa ishacheza mechi 12 na kushinda 3,
imefungwa 7 na kutoa sare mechi 2 haikuwa rahisi kupata matokeo licha ya
kuwa ilikuwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge London.
Hadi dakika 90 zinamalizika Chelsea walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 licha ya kukosa nafasi kadhaa, goli la Chelsea lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu hiyo Diego Costa dakika ya 64 ya mchezo na kuwatuliza mashabiki wa Chelsea waliokuwa hawana furaha kutoka na mfululizo wa matokeo mabovu.
Matokeo ya mechi nyinine za Ligi Kuu Uingereza Zilizochezwa November 21
-
Watford 1 – 2 Manchester United
-
Everton 4 – 0 Aston Villa
-
Newcastle United 0 – 3 Leicester City
-
Southampton 0 – 1 Stoke City
-
Swansea City 2 – 2AFC Bournemouth
-
West Bromwich Albion 2 – 1 Arsenal
0 comments:
Post a Comment