Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars November 17 ilicheza mchezo wake wa pili wa marudiano ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi dhidi ya Algeria Blida katika uwanja wa Mustapha Tchaker na kukubali kipigo cha magoli 7-0, idadi ya magoli ambayo iliifanya Tanzania kuingia katika headlines ya ya kufungwa idadi kubwa ya magoli.
November 18 kocha wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa
ameongelea namna alivyokipokea kipigo hicho na kufanya kiweke historia
kwake kwani kwa miaka yake 25 katika soka hakuwahi kuweka rekodi ya
kupokea kipigo cha magoli mengi kiasi hicho kitu ambacho hakikuwaumiza
watanzania hata yeye.
“Kiukweli
hata mimi ilinishangaza kidogo na tulizidiwa umeona uwezo wa mchezaji
wao Yacine Brahimi uwezo wake ni mkubwa kikosi chao kilibadilika ila
uwanja pia ulikuwa tatizo ulikuwa unateleza hata goli la kwanza
tulilofungwa lilitokana na hivyo, kufungwa goli 7 sijawahi kiukweli
katika miaka 25 yangu katika soka” >>> Boniface Mkwasa
0 comments:
Post a Comment