Hii taarifa tayari imeripotiwa
mitandaoni na kwenye vyombo vingi vya habari kutoka Mkoa wa Morogoro
ambapo inahusu kutolewa kwa hukumu ya Sheikh Issa Ponda ambaye ameachiwa huru baada ya kukutwa hana hatia.
Sheikh Issa Ponda alishtakiwa
kwa makosa matatu ikiwemo kukiuka amri ya Mahakama kufanya mkusanyiko
pamoja na kutoa maneno ya uchochezi… Mawakili wa Sheikh Issa Ponda wamesema waliamini haki itatendeka japo imechelewa.
Baada ya hukumu hiyo, Sheikh Ponda aliondoka kuelekea kwenye Msikiti wa ‘MUNGU Mmoja Dini Moja‘ uliopo Morogoro kwa ajili ya kuongea na waumini wake.
0 comments:
Post a Comment