Taarifa kuhusu upotoshaji wa mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015.
Taarifa kwa vyombo vya Habari , 4 Aprili 2015
Taarifa kuhusu upotoshaji wa mswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015
Naomba
nifafanue kuhusu propaganda inayoenezwa na maafisa wa TCRA kupitia
CloundsFM kuhusu Sikika na Mswada wa #CyberCrimeBill.
Sikika haikuhudhuria mkutano wa wadau unaodaiwa kufanyika Dodoma kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na leo maafisa wa TCRA.
Sikika
haikutoa maoni kuhusu Mswada wa miamala ya kielektoniki kama
ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na pia leo maafisa wa TCRA.
Sikika
ilituma maoni ya pamoja ya wadau kwa niaba ya wadau kuhusu
#CyberCrimeBill kwa njia ya email kwa Mkiti Kamati Mh Peter Serukamba.
Maoni
hayo hayakutumika kuboresha #CyberCrimeBill bali kuongeza tu orodha ya
wadau wanaoda iwa "kushiriki" kwa lengo la kuonesha kuridhia.
Kwa
kuwa maoni ya wadau hayakuzingatiwa na kwamba #CiberCrimeBill
iliyopitishwa ina mapungufu mengi, Sikika na wadau bado wanaipinga.
Mwisho tunaomba jina la Sikika lisiendelee kutumika kuhalalisha upitishwaji wa sheria hii.
Irenei Kiria
Mkurugenzi wa Sikika
4 Aprili 2015.
4 Aprili 2015.
0 comments:
Post a Comment