Home » »

Wanafunzi 147 wauawa kwenye Shambulizi la Garissa

Waziri wa Usalama wa Taifa nchini Kenya, Joseph Nkaissery, ametangaza kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na shambulizi la kigaidi katika chuo kikuu cha Garissa, mashariki mwa Kenya ni 147. Waziri Nkaissery amesema kwenye tukio hilo zaidi ya watu 75 wamejeruhiwa wakiwemo maafisa wa polisi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon mapema leo amelaani shambulizi la kigaidi dhidi ya chuo kikuu katika mji wa Garissa.  Ban amesema ni jambo lisilokubalika kwa watu kuwavamia walimu na wanafunzi na kuwaua bila hatia. Mkuu huyo wa UN ametaka juhudi zote zifanywe ili kuwakamata wahusika na kuwaadhibu kwa mujibu wa sheria.
Mapema leo alfajiri, watu wenye silaha walivamia Garissa University College na kuanza kufyatua risasi ovyo. Habari zinasema watu hao wamewashikilia mateka wanafunzi kadhaa. Serikali ya Kenya imesema itahakikisha kadhia hiyo inashughulikiwa kwa ustadi mkubwa ili kuepusha kuuawa raia wasio na hatia lakini pia kwamba itafanya juu chini kuwaadhibu waliohusika. Kundi la al-Shabab limetoa taarifa na kudai kuhusika na shambulizi hilo. Msemaji wa kundi hilo Ali Mohammed Rage ameliambia shirika la habari la AFP kuwa wapiganaji wa kundi lake wametekeleza hujuma hiyo na bado wako katika eneo la tukio. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya imesema gaidi mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akijaribu kukimbia.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog