Vyama Vingi vya Siasa Vinatamaa ya Madaraka na Vyeo - Zitto Kabwe
Kiongozi
Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and Transparency ACT Wazalendo,
Zitto Kabwe, amesema kuwa vyama vingi vya siasa nchini,vinasumbuliwa na
uroho wa madaraka pamoja na vyeo.
Aliongeza
kuwa vyama hivyo katika mikutano yake vimekuwa vikiacha kueleza
matatizo yanayowakabiliwananchi badala yake ni kutukana mwanzo mwisho.
Zitto
alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wakazi wa Mji wa Maswa
mkoani Simiyu, katika uwanja wa Madeco, wakati wakihitimisha ziara
yakukitambulisha chama katika mikoa 12 nchini.
Alisema
uroho wa kutaka madaraka na vyeo kwa baadhi ya wanachama na viongozi wa
vyama hivyo, limekuwa tatizo kubwa na kuvifanya kushindwa kupambana
kutetea hali za Watanzania ambao niwengi wao ni maskini wa kupindukia.
“Baadhi
ya vyama vya siasa hapa nchini kazi yao ni matusi tu katika mikutano
yao pamoja na kutambiana, vinashindwa kuwaeleza wananchi wanavyonyonywa
na rasilimali zao zinavyonufaisha wachache, lakini pia tamaa ya madaraka
pamoja vyeo katika vyama hivyo ni tatizo,” alisemaZitto.
0 comments:
Post a Comment