HIZI NDIZO MALI ZA HATARI ZILIZOMZIMISHA GWAJIMA WAKATI AKIHOJIWA NA POLISI, WAUMINI WAKE WANENA MAZITO.
KWA wiki moja sasa,
baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kwamba, kujisikia
kizunguzungu hatimaye kuanguka na kupoteza fahamu kulikomtokea Mchungaji
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima wakati akihojiwa na
polisi kulitokana na kuulizwa maswali yaliyohusu namna alivyozipata mali
zake, Risasi Jumamosi linakupa zaidi.
Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.
Machi 28, mwaka huu
Mchungaji Gwajima alipojisalimisha Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maaalum
ya Dar es Salaam kwa madai ya kumtolea maneno yenye kuudhi Askofu wa
Kanisa la Romani Katoliki Jimbo Kuu la Dar, Mwadhama Polycarp Kadinali
Pengo, alijikuta akizidiwa ghafla na kukimbizwa Hospitali ya TMJ kwa
matibabu huku akiwa amepoteza fahamu.
Ilidaiwa kuwa, Gwajima
alipokwenda kituoni hapo kujisalimisha alitarajia kukutana na mahojiano
ya kuhusu kauli yake ya kumkashifu Kadinali Pengo, lakini matokeo yake
akakumbana na maswali ya kuhusu mali zake.
WALIVYOSEMA WATU
“Unajua Gwajima yeye
alipoambiwa ajisalimishe Central kwa kumkashifu Pengo alijua akifika
pale ataulizwa kwa nini ulimtusi Pengo? Alikukosea nini? Huoni kama yule
ni mtu mzima kuliko wewe? Je, uko tayari kumwomba radhi? Lakini matokeo
yake katikati ya maswali akaulizwa mali alizonazo alizipata kwa njia
gani?”
KWA NINI ALIZIMIA SASA?
Gari lake la kifahari.
“Sasa suala siyo kwamba
swali hilo la kuhusu mali lilikuwa na shida kwake, bali lilikuwa la
ghafla ndiyo maana akajikuta akichanganyikiwa na kupoteza fahamu,”
kilisema chanzo kimoja.“Wengi wanasema alipoulizwa kuhusu mali alizimia
kwa sababu mali zenyewe si halali, hapana! Zile mali ni halali kabisa
ila swali halikuwa kwenye mawazo ya Gwajima,” kiliendelea kusema chanzo.
RISASI JUMAMOSI LAZICHIMBA
Kufuatia madai hayo,
Risasi Jumamosi liliamua kuzama kazini na kuzichimba mali hizo kwa nia
ya kuzitambua ambapo uchunguzi wa kina uliofanywa ulibaini kwamba,
Mchungaji Gwajima anamiliki gari la kifahari aina ya Hummer 2 ambalo
gharama ya manunuzi mpaka kufika Tanzania ni wastani wa shilingi milioni
250.
Mbali na gari hilo la
kifahari, Gwajima amewanunulia wachungaji wake 30 magari ya kutembelea
ili kupambana na tatizo la usafiri jijini Dar.
Nyumba yake ya kifahari.
MAGARI YAANIKWA
Baadhi ya magari hayo ni
Subaru Forester (sokoni linauzwa shilingi milioni 17), Mitsubishi
Pajero (shilingi milioni 16), Toyota Spacio new model (milioni 20) na
Toyota Harrier Lexus (milioni 35).
MJENGO WA MAANA
Risasi Jumamosi
lilibaini pia kuwa, mchungaji huyo anaishi kwenye nyumba yake ya
kifahari ya ghorofa nne iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.
Helkopta yake.
MABASI 20
Kweli Gwajima ni tajiri
kwani Risasi Jumamosi likabaini kuwa, pia anamiliki mabasi 20 ambayo ni
kwa ajili ya kuwabeba waumini wa kanisa lake wakati wa kwenda kwenye
ibada na kurudi makwao katika sehemu mbalimbali za Jiji la Dar. Mabasi
hayo kila moja alilinunua kwa shilingi milioni mia moja na ishirini.
PIA KUNA HELKOPTA
Pia, miezi ya hivi
karibuni, Gwajima alinunua helkopta (chopa) kwa ajili ya kuzungukia
sehemu mbalimbali nchini kutoa huduma ya kiroho. Uzinduzi wa helkopta
hiyo ulifanywa na mbunge wa Monduli (CCM) na waziri mkuu wa zamani,
mheshimiwa Edward Lowassa.
Magari ya wachungaji.
ANAONGOZA KWA KUWA NA WAUMINI WENGI
Uchunguzi pia ulibaini
kwamba, Kanisa la Mchungaji Gwajima linaongoza kwa kuwa na waumini wengi
ambapo wanakadiriwa kufikia 70, 000. Kwa maana hiyo sasa, kama waumini
wake watatoa sadaka ya Jumapili kila mmoja kwa shilingi elfu mbili,
atakuwa anaingiza shilingi milioni 140 kwa ibada moja.Kwa mwezi, Gwajima
atakuwa anaingiza shilingi milioni 560 japokuwa wapo waumini inadaiwa
hutoa hadi shilingi laki tano (500,000) kama sadaka kwa ibada moja.
MSAMAHA WA KODI
KWA mujibu wa sheria za
nchi, baadhi ya taasisi zimepewa msamaha wa kodi wakati wa kuingiza
bidhaa mbalimbali nchini, hasa zinazohusu huduma kwa jamii. Bidhaa hizo
ni pamoja na magari (Tax Exemption).
Taasisi hizo ni pamoja na za dini, elimu, afya (madaktari) na nyingine zenye kuhudumia jamii.
Magari ya kubebea waumini.
“Kwa hiyo Gwajima
anaweza kumiliki mali nyingi kwa sababu anao msamaha wa kodi, anaweza
kuingiza magari mengi kwa kodi ndogo sana,” alisema mmoja wa waumini wa
Kanisa la Gwajima.
MKEWE ANASEMAJE?
Kwa mujibu wa mke wa
Gwajima, Grace alipozungumza na vyombo vya habari hivi karibuni, alisema
suala la mumewe kuzimia waulizwe polisi.“Mume wangu aliondoka mzima
kabisa, polisi ndiyo waulizwe kwa nini alizimia.”
0 comments:
Post a Comment