Majambazi Yavamia Kanisani na Kuiba Chombo Kinachotumika Kuhifadhia Ekaristi Takatifu......Kwa Mujibu wa Sheria Za Roma, Ukristo Ndo Basi Tena Eneo Hilo
Watu watano wamevamia na kuvunja madirisha ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Malolo na kuiba chombo kinachotumika kuhifadhia ekaristi takatifu (TABERNACULO).
Imeelezwa kuwa majambazi hayo yalidhani chombo hicho kimetengenezwa kwa dhahabu.
Tukio hilo lilitokea juzi, saa 8:30 usiku, baada ya majambazi hayo kuvunja madirisha ya kanisa hilo.
Kanisa hilo ni miongoni mwa makanisa makongwe na yenye historia kubwa hapa nchini, ambalo lilijengwa mwaka 1939.
Paroko wa
kanisa hilo, Theophan Membe, alisema siku ya tukio alikuwa Lindi
kuhudhuria misa takatifu ya mapadre wa jimbo la Lindi, iliyoongozwa na
Askofu wa jimbo hilo Mhashamu Bruno Ngonyani.
Alisema baada
ya tukio hilo alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kigango cha Malolo,
Cleophas Nnonjela, na badaye walitoa taarifa polisi.
Membe alisema parokia ya Malolo ni miongoni mwa parokia zilizotoa wasomi wengi mkoani Lindi kutokana na historia yake.
Alisema kwa
mujibu wa sheria za Roma za kanisa hilo, sehemu inayoibiwa Tarbenaculo,
ukristo hufa mpaka wahusika walioiba kifaa hicho watakapokiri kuwa
wameiba.
Membe alisema
baada ya wahusika kukiri kama wameiba, askofu wa jimbo anaondoa dhambi
ya mauti kutoka kwa waumini kwenda kwa wezi hao.
Alisema
kutokana na kuibiwa kifaa hicho, waumini wa kigango hicho watakosa
baadhi ya huduma ikiwemo ibada ya Jumapili, misa ya kila siku asubuhi,
misa ya katekista na upigwaji wa kengele zinazoashiria saa kwa waumini.
Alisema katika
kipindi hicho huduma za ubatizo, kipaimara, komunio takatifu, kitubio,
misa za mazishi, mpako kwa wagonjwa, sherehe za ndoa na masuala yote ya
msingi yanayohusu Kanisa Katoliki hayatakuwepo.
PAROKO wa kanisa katoliki parokia ya Malolo padre THEOPHANI MEMBE
ambaye ameonesha kukerwa na kitendo kilichofanywa na Watu hao ambao
mpaka sasa hawajulikani huku akiahidi kusitisha huduma ya ibada kwenye
kigango hicho.
KANISA Takatifu la Mtakatifu JOSEPH
MFANYAKAZI Parokia ya Malolo Jimbo la Lindi katika mkoa wa Lindi ambamo
TARBENACULO hilo limeibiwa na watu wasiofahamika.
NYUMBA anayoishi Paroko wa parokia ya Malolo Fr.Theophan Membe
ambayo Mlango wake kwa huko nyuma umevunjwa na watu wasiofahamika
waliokuwa na lengo la kuiba.
ASKOFU wa Jimbo la Lindi Mhashamu
BRUNO NGONYANI ambaye anasubiriwa kutangaza adhabu kwa waumini wa kanisa
katoliki kigango cha Malolo wakati wowote kutoka sasa mpaka pale
waliohusika watakapokiri mbele ya waumini.
0 comments:
Post a Comment