UTAMADUNI wa wananchi kujichukulia sheria
mkononi unazidi kushabikiwa na kuchochea ghasia kila mahali nchini hali
inayoweza kusababisha madhara makubwa pamoja na uvunjifu wa amani.
Siku moja baada ya madereva kugoma na
kusababisha hadha kubwa kwa abiria na watumiaji wa vyombo vya usafiri katika
maeneo mbalimbali nchini na hasa hasa jijini Dar es Salaam kulikoshuhudiwa
jeshi la Polisi likilazimika kutumia mabomu ya machovu kuwatawanya waliokuwa
wanafanya fujo, kuchoma matairi barabarani na hata kuiba mali na kuharibu
magari ya watu wengine wakati mgomo huo ukiendelea:
Leo hii katika eneo la stendi ya Ipogolo,
vijana wenye hasira kali wamechoma matairi chakavu barabarani na kusababisha
usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara iendayo katika stendi hiyo, baada ya dereva
na gari ambalo hata hivyo halikujulikana mara moja kumgonga mtoto aliyekuwa
akivuka barabara hiyo na kufariki papo hapo.
0 comments:
Post a Comment