Kesi Ya Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Nchini, Johnson Minja Kuanza Leo Ambapo Atasomewa Maelezo Ya Awali Ya Kesi Yake.
Kesi ya kushawishi wafanyabiashara wasilipe kodi kwa serikali inayomkabili Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Nchini, Johnson Minja inaanza kusikilizwa leo.
Kesi
hiyo iko katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini mbele ya Hakimu
Mkazi, Rebecca Mbilu ambapo leo itaanza usikilizwaji kwa mshtakiwa
kusomewa maelezo ya awali ya kesi yake.
Mshitakiwa
huyo ambaye yuko nje kwa dhamana anakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo
la kuchochea wafanyabiashara wasilipe kodi ya serikali.
Upande
wa mashtaka kuiongozwa na Wakili wa Serikali, Godfrey Wambali ulidai
kuwa, Septemba 6, mwaka jana wakati Minja alipokuwa katika mkutano na
wafanyabiashara uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Mjini hapa
mshitakiwa alitenda makosa mawili ya kushawishi wafanyabiashara
wasilipe kodi na kuzuia ukusanyaji wa kodi kwa kutumia mashine za
kielektroniki (EFDs).
Upande
wa mashtaka ulidai kitendo alichofanya mshtakiwa ni kinyume na kifungu
cha 390 kinachosomeka pamoja na kifungu cha 35 cha Sheria ya kanuni ya
adhabu sura ya 16 ni kosa kushawishi vitendo vyovyote vya jinai.
Alidai
hata kifungu cha 107 kifungu kidogo cha Sheria ya kodi sura ya 332 ya
mwaka 2004 ni kosa kuzuia ulipaji wa kodi kwa Serikali. Mshitakiwa
alikana mashtaka hayo. Minja anatetewa na wakili wa kujitegemea Godfyey
Wasonga.
0 comments:
Post a Comment