BODABODA AFA KWA KUCHINJWA, NDUGU WAZIKA MGOMBA, UTATA WATAWALA
TUKIO la aina yake!
Dereva wa bodaboda aliyejulikana kwa jina la Alex Wilson amekutwa
ameuawa kwa kuchinjwa na kuporwa pikipiki lakini cha ajabu, siku ya
mazishi yake kaburini kukazikwa mgomba baada ya mwili kuzuiwa usizikwe,
Uwazi limechimba kisa kamili.
Marehemu Alex Wilson enzi za uhai wake.
Ilikuwa Aprili 8, mwaka
huu katika maeneo ya Mbezi Beach karibu na Kiwanda cha Rafia, Alex
ambaye ni mwenyeji wa Sumbawanga mkoani Rukwa, aliuawa kwa kuchinjwa
mfano wa kuku.Baada ya kifo hicho, madereva bodaboda wenzake waliungana
na kutafuta ndugu wa karibu ili kuwajulisha kilichomkuta Alex.
Inadaiwa kuwa, katika
kutafuta alikokuwa akiishi marehemu huyo, wenzake walifanikiwa kupapata
na kumkuta mtoto wa mama mwenye nyumba ambapo walimuonesha picha za enzi
za uhai wa Alex naye ndugu huyo alikiri kwa kusema ni kaka yake.
Walimuuliza mtoto huyo aliko mama yake akasema yuko safarini Sumbawanga kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka.
“Tulimwomba namba ya
simu ya mama yake, akatupa. Tulipompigia alisema kweli anamtambua
marehemu lakini yeye yuko Sumbawanga,” alisema mmoja wa madereva
bodaboda hao.
Wananchi wakipeleka mgomba makaburini.
Inadaiwa kuwa, bodaboda
hao walimtaka mama huyo kutoa tamko juu ya kuusafirisha mwili wa Alex
kwenda Sumbawanga au kuuzika jijini Dar ambapo alisema waende serikali
ya mtaa kwa ajili ya kupata utaratibu kisha wamzike.
“Siku iliyofuata, yaani
Aprili 9, mwaka huu, tukiwa na baadhi ya ndugu wa mbali wa Alex
tulikwenda Kituo cha Polisi Afrikana (Dar) kuomba kibali cha mazishi,
lakini ikabidi polisi wafanye mawasiliano na yule mama aliye Sumbawanga.
“Polisi walimpigia simu
na kuweka loud speaker (spika kwa sauti ya nje) wakimtaka mama huyo
afike Dar haraka kwa mazishi ya mtoto wake au waruhusu mtoto wake
azikwe.“Lakini yule mama alijibu kuwa, wasijaribu kufanya kitendo
chochote cha mazishi kwa vile anajua kuwa mwanae huyo hajafa na
anajua alipo.
Kaburi likiandaliwa kwa ajili ya mazishi.
“Mama alisema watu
wakifanya lolote watakiona maana yeye anatoka Sumbawanga, hivyo zoezi la
kuendelea na taratibu za maziko zikakwamia hapo,” alisema bodaboda
mmoja.Aliendelea kusema kuwa, wakati wanafanya utaratibu wa kupata
kibali tayari walishachimba kaburi kwa ajili ya kumhifadhi marehemu.
“Lakini baada ya mama kujibu vile, polisi walifanya mawasiliano na
viongozi wa juu na kuzuia maziko hadi ndugu sahihi wapatikane na hivyo
mwili wa maremu upo Hospitali ya Mwananyamala (Dar) ukisubiri.”
Baada ya hapo bodaboda
hao kwa kushirikiana na ndugu wa mbali, walilazimika kukata mgomba na
kuuzika kaburini badala ya mwili wa marehemu.Mgomba huo ulizikwa katika
Makaburi ya Kinzidi, Aprili 9, mwaka huu kwa kile kilichodaiwa kuwa,
kuacha kaburi wazi wakati lilishachimbwa kwa ajili ya maziko ni uchuro
kwa wengine walio hai.
Mgomba ukiwa kwenye kaburi.
Jumamosi iliyopita,
Uwazi lilifanya jitihada na kumpata mama huyo kwa njia ya simu ambapo
alijitambulisha kwa jina la mama Dickson na kusema yupo Mtaa wa Majengo
wilayani Sumbawanga, Rukwa.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na marehemu Alex, mwanamke huyo alisema:
“Ni kweli Alex namfahamu
na tulifahamiana Dar es Salaam na hii ni kutokana na kunifahamu mimi ni
mtu wa Sumbawanga hivyo siku za nyuma alikuja nyumbani kwangu na
kujitambulisha, mimi nilimchukulia kama mwanangu.
Mgomba ukifukiwa.
“Ilifika mahali akawa
ananiita shangazi, mahusiano yalikuwa ni makubwa kutokana na kutoka
sehemu mmoja yeye alinichukulia kama ndugu yake wa karibu.“Mbali na
kutoka sehemu mmoja sina undugu na Alex.”
0 comments:
Post a Comment