Watu Sita Wakamatwa Na Jeshi La Polisi Kwa Tuhuma Za Kumbaka Mwanamke Mmoja Kwa Zamu.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Juma Saad Khamis, alisema hilo ni moja
ya matukio mabaya kuripotiwa kufanywa katika kipindi cha maadhimisho ya
sikukuu ya Pasaka.
“Watu hao walikamatwa Jumapili saa 2 usiku wakihusishwa kuhusika na tukio hilo,” alisema.
Uchunguzi
wa awali unaonesha kuwa siku ya tukio watuhumiwa walionekana wakinywa
na mwanamke huyo na baadaye walianza kumpiga na kumchukua hadi maeneo ya
Bwejuu.
Hata
hivyo Kamanda Khamis alikataa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na
watuhumiwa hao kwa maelezo kuwa yanaweza kuvuruga upelelezi wa tukio
hilo ambao unaendelea kufanywa na mamlaka husika.
Alisema ukiacha tukio hilo baya, wananchi walisherehekea kwa amani sikukuu ya Pasaka.
“Kulikuwa na amani, nawashukuru polisi wa doria kwa kazi yao nzuri na kusababisha wananchi kusherehekea sikukuu kwa amani,” alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Mkadam Khamis Mkadam.
Kamishna
Msaidizi (ACP) Mkadam alisema kulikuwa na matukio madogo ya ajali za
barabarani, naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mohamed
Msangi alisema katika mkoa wake hakukuwa na matukio mabaya.
0 comments:
Post a Comment