HOT NEWS..!! MVUA KUBWA YA RADI YAUA WATU 8 HUKO KIGOMA YUMO MWALIMU NA WANAFUNZI 6
Mwalimu Merina Sekilo aliyenusurika kupigwa na radi wakati akifundisha darasa la kwanza,ambapo wanafunzi 6 walifariki dunia
Mwalimu
Veronika Mtes wa shule ya msingi Kibirizi aliyepata mshtuko baada ya
tukio la radi akiwa katika hospitali ya Maweni mkoa wa Kigoma kwa
matibabu.
WATU
wanane wakiwemo wanafunzi sita na mwalimu wa shule ya msingi Kibirizi
pamoja na mkazi wa eneo la Bangwe mjini Kigoma wamefariki dunia baada
ya kupigwa na radi huku wanafunzi wengi 15 wakijeruhiwa na radi hiyo
leo mchana.
Mganga
mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa kigoma(Maweni)Dkt Fadhili Kabaya
amesema kuwa watu hao walifikwa na mauti hayo kufuatia mvua kubwa
zilizonyesha zikiambana na radi zilizoanza majira ya saa sita mchana.
Dkt
Fadhili amewataja waliopoteza maisha katika tukio hilo kuwa ni pamoja
na mwalimu wa shule ya msingi Kibirizi Elinaza Mbwambo(25) na Forcus
Ntahaba(45)mkazi wa eneo la Bangwe mjini Kigoma.
Amewataja
wanafunzi waliofariki dunia ambao wote ni wa darasa la kwanza kuwa ni
Yusuph Ntahoma(8)Hassan Ally(9)Fatuma Sley(7)Zamda Seif(8)Shukrani
Yohana(7) na Warupe Kapupa(10).
Amesema
wamepokea majeruhi kumi na tano lakini kati yao kumi wametibiwa na
kuruhusiwa kurudi nyumba baada ya hali zao kuwa nzuri na watano
wamelazwa wanaendelea na matibabu katika hospital ya Mkoa wa Kigoma.
Akisimulia
tukio hilo mwalimu aliyekuwa anafundisha darasani Mwalimu Merina Sililo
amesema akiwa darasani akiendelea kufundisha ghafla aliona wingu zito
jeusi limetanda hadi akashindwa kuendelea kuandika ubaoni.
''Manyunyu
yalianza kidogo kidogo ikaja mvua kubwa na radi pamoja na miungurumo
mikali sana ,iliyopelekea wanafunzi kuanguka ovyo darasa na kuzimia ,na
mara niliona moto umetanda katika chumba kuzima cha darasa na mimi
nilianguka chini na kupoteza fahamu''amesema mwalimu huyo.
Amesema
apozinduka alijikuta katika hospitali ya Mkoa ya maweni akipatiwa
matibabu baada ya kuletwa kwa msaada wa waalimu wenzake.
''Kwa
kweli ni mungu tu mwenyewe ndiyo ameninusuru kwani nilirushwa mara tatu
na radi na watoto wote wote darasani walikuwa wananiangukia mimi
wengine walikuwa wanakimbia ovyo nje'',amesema Mwalimu huyo.
0 comments:
Post a Comment