POLISI, MAJAMBAZI WARUSHIANA RISASI, WAWILI WAUAWA
WATU wawili akiwemo jambazi mmoja wamefariki
dunia na wengine kunisurika kuuawa katika tukio la lililotokea juzi, mjini
Mafinga mkoani Iringa wakati majambazi yakirushiana risasi na askari wa jeshi
la Polisi.
Risasi hizo zilipigwa wakati Polisi
hao wakijaribu kuokoa fedha za mfanyabiashara Salama Semwaiko zilizoporwa na majambazi
wawili waliotumia pikipiki wakati wakifanya uporaji huo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa,
Ramadhani Mungi alisema mfanyabiashara huyo aliporwa fedha hizo juzi majira ya
saa 2.45 asubuhi alipokuwa akitoka nyumbani kwake kwenda kwenye biashara zake.
Tukio hilo la kusikitisha lilovuta
hisia za watu wengi na kufanya baadhi kuzimia wengine kukimbia hovyo
na kujifungia ndani kwa ajili ya kuokoa maisha yao lilitokea
katika eneo la Kinyanambo B, nje kidogo ya mji wa mafinga.
Kamanda Mungi alisema “akiwa katika
gari yake akielekea kwenye biashara zake mjini mafinga, mfanyabiashara huyo alisimamishwa na mtu mmoja
aliyekuwa amevaa koti jeusi na baada ya kusimama alimtolea silaha na kumtaka
atoe fedha na vitu vyote vya thamani alivyoko navyo .”
“Baada ya kuona hana msaada
mfanyabiashara huyo alijikuta akilazimika kutoa Sh 700,000 alizokuwa nazo, simu
ya mkononi na baadaye ilitokea pikipiki ambayo haikufahamika namba za usajili
na kumpakia mtu huyo na kuanza kukimbilia eneo la kinyanambo,” alisema.
Alisema mara baada ya majambazi hao
kutoweka jeshi la polisi lilipewa taarifa na kuwahi eneo la tukio na kwa
kushirikiana na wanachi walianza kuwakimbiza majambazi hao na ndipo majibizano
ya risasi yalipoanza.
Katika hekaheka hiyo, Kamanda Mungi
alisema Said Ngudi (25) ambaye ni mwanajeshi wa JKT Makutopola aliuawa kwa
bahati mbaya wakati akisaidia kupambana na majambazi hao.
“Kijana huyo alipigwa risasi ya kifuani
upande wa kushoto na kufariki dunia papohapo lakini wanachi
wananchi na askari hawakurudi nyuma kwani waliendelea kupambana na majambazi hao,”
alisema.
Kamanda Mungi alisema katika
majibishano hayo hatimaye polisi walifanikiwa kumpiga risasi ya kwenye paji la
kushoto jambazi aliyempora mfanyabiashara huyo na hatimaye wanachi walimvania na
kumpiga kwa mawe kabla hajaokolewa na kufariki dunia wakati akipatiwa
matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.
Katika tukio hilo ambalo jambazi
mmoja aliyekuwa akiendesha pikipiki alitokomea kusikojulikana, jeshi la polisi lilifanikiwa kukamata bunduki moja
aina ya SMG na kuwashukuru wanachi kwa ushirikiano wao katika ulinzi shirikishi.
0 comments:
Post a Comment