ASKOFU MWASOTA AVUNJA UKIMYA TUHUMA ZA KUNASWA NA KUNDI LA FREEMASON
Askofu David Mwasota, katibu wa baraza la makanisa ya kipentekoste nchini CPCT. |
Hatimaye
Katibu Mkuu wa Baraza la makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT)
Askofu David Mwasota, amevunja ukimya wa tuhuma zilizosambazwa sehemu
mbali mbali zikieleza kuwa amenaswa na kundi la siri la waabudu shetani
Freemasons.
Akiongea na chanzo cha habari cha blogger kwa uchungu, Askofu Mwasota alisema:
“Ndugu
yangu naona haya ni mashambulizi, nimezushiwa mengi achilia mbali
yaliyoandikwa na magazeti, jumbe zinasambazwa kwa watumishi wa Mungu
(wachungaji) wakae mbali na mimi eti nimekuwa freemason, lakini haya
yote ni mashambulizi tu…”
Akifafanua
zaidi alisema: “Nakwambia ukweli kutoka moyoni mwangu, sijui hata
kiongozi mmoja wa kundi la Freemasons, wala sijui hata hekalu lao liko
wapi, mimi nilikuwa nafundisha kanisani nikawaonya wapentekoste wakae
mbali na watu wasiowajua kwa kuwa wengine ni waabudu shetani, na
wanawajia kama watu wema ili kuwarubuni,”alisema kiongozi huyo na
kuongeza:
“Nikatoa
mfano wa waumini wangu na mimi mwenyewe, nakumbuka niliwaambia kuwa
niliwahi kuhudhuria semina moja na baada ya kukamilika nilipewa nishani
ambayo baadaye nilikuja kubaini kuwa ilikuwa na nembo nisisozielewa,
sikusema ni nembo za Freemasons, nilisema nisizozielewa, nikaamua
kuitupa hiyo nishani, lakini naona waandishi waliamua kunimaliza,
namwachia Mungu aamue kati yetu…”
Alipoulizwa ni semina gani hiyo na kama anauhakika kuwa nembo alizoshtukia sio za kundi hilo, alijibu:
“Sikia
ndugu…nilichosema kilikuwa ni mfano tu wakati nahubiri, nilimaanisha
kuwa nembo hizo sikuwa na uhakika nazo, hiyo haimaanishi zilikuwa ni za
kundi la Freemasons, nimekwisha kueleza sijui hata kiongozi mmoja wa
kundi la Freemasons, wala sina haja nao, mimi nimeokoka naenda mbinguni
waabudu shetani ni wanini?”
“Jambo
la kustaajabisha zaidi ni kuwa wewe ndio Mwandishi wa kwanza kuongea
nami, kuhusu jambo hili kwa mapana yake, wengine walinipigia simu
nikawaambia waje ofisini sikuwaona, lakini nikashtukia habari kubwa
imeandikwa, hii inaniuma sana…”
Askofu
Mwasota, alisema kuwa ameshauriwa juu ya jambo la kufanya na anajiandaa
kuchukua hatua kwa kuwa anaona kuwa kuna njama mbaya dhidi yake, huduma
anayoiongoza na kanisa la Mungu kwa ujumla.
Alisisitiza
kuwa katika ibada hiyo lengo la mahubiri yake lilikuwa ni kuwaonesha
wapentekoste hatari iliyopo mbele yao kwa kuwa makundi hayo ya waabudu
shetani yapo na yanawawinda.
“Mimi
ni Askofu na kiongozi wa baraza la Wapentekoste, ilikuwa ni wajibu
wangu kuonya wenzangu, lakini mifano yangu ilipinduliwa kwa makusudi.
Nadhani wakati nahubiri kulikuwa na mwandishi wa (jina linahifadhiwa)
ambaye aliichukua kama alivyotaka,” alisema Askofu Mwasota.
Kwa
karibu wiki nzima kumekuwa na jumbe mbali mbali zinazosambazwa kupitia
simu zikieleza kuwa Askofu Mwasota amenaswa na kundi la Freemasons na
kuwataka wapentekoste kukaa mbali naye.
Baadhi
pia ya waumini wa makanisa ya Kipentekoste na hata wachungaji wamekuwa
wakiulizana huku na kule wakitaka ukweli kuhusu habari za kiongozi huyo
wa ngazi ya juu katika baraza la Wapentekoste kutajwa na kundi hilo.
Kutokana
na kiu hiyo ya watu wa Mungu, Blog hii liliamua kuchunguza ukweli wa
jambo hilo kuanzia kwa Askofu mhusika na vyanzo vingine vya habari ili
kutoa jibu kwa wenye kuguswa na mkanganyiko huo.
Baadhi
ya watu wa karibu na Askofu Mwasota, waliofanya mahojiano ya siri
nachanzo kimoja cha blog wameeleza wasi wasi wao kuwa kuenea kwa kasi
kwa habari hiyo na mazingira yake vinaashiria kuwa huenda kuna mbegu ya
chuki inayochochea jambo hilo.
Mmoja
wa watu waliohudhuria ibada siku Askofu Mwasota alipohubiri na kuwaonya
watu kukimbia makundi ya wale wanaowajia ghafla kama malaika wa nuru,
alisema:
“Mimi
nilikuwa kwenye ibada siku Askofu Mwasota alipohubiri na kutoa mifano;
nilichosikia akisema ni kuwa alihudhuria semina na mwisho akapewa
nishani ambayo baadaye alibaini kuwa na nembo, ambazo hakuwa na uhakika
nazo na kwa kutotaka kujichanganya akaamua kuitupa, wala hakusema kuwa
amehudhuria mkutano wa Freemasons.”
Katika
siku za karibuni kumekuwa na mlipuko wa makundi ya vijana wanaosaka
jinsi ya kujiunga na kundi la Freemasons wakidai eti ni suluhisho la
maisha magumu.
Habari
za kuenea kwa kasi kwa kundi la Freemasons zimekuwa zikivuta hizia za
watu wengi, wengine wakidhani kuwa kujiunga nao kunaweza kuwafanya kuwa
tajiri.
0 comments:
Post a Comment