Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRGG) imelaani hatua
zilizoripotiwa kuchukuliwa na baadhi ya wakuu wa Mkoa na wakuu wa wilaya
kuwaweka selo watumishi ambao wameshindwa kutimiza majukumu yao ya
kikazi.
Kwa
mujibu wa tamko lililotolewa juzi na mwenyekiti wa CHRGG, Bahame
Nyanduga, kamisheni hiyo ilipokea ripoti ya vitendo vya baadhi ya wakuu
wa mikoa na wakuu wa wilaya kutoa amri za kuwakamatwa na kuwekwa selo
kwa muda fulani watumishi wa umma.
Mwenyekiti
huyo alieleza kuwa makosa ya kiutendaji yanapaswa kuchukuliwa hatua za
kiutendaji kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma na sio kuwaweka jela
kama watu waliofanya makosa ya jinai.
Taarifa
hiyo ilitaja baadhi ya matukio ambayo imepokea ripoti zake kuwa ni
pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuamuru maafisa
ardhi waliochelewa kufika kazini wakamatwe na kuwekwa selo kwa saa 6.
Alilitaja
tukio lingine kuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma kuamuru afisa afya wa
kata kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa kosa la kutosimamia ipasavyo
utekelezaji wa maelekezo ya rais John Magufuli, kufanya usafi katika
siku ya kumbukumbu ya Uhuru, Disemba 9.
“Kuwapa adhabu za kinidhamu ingekuwa njia bora zaidi kuliko kuwafunga jela kama wamefanya jinai,” inasomeka sehemu ya tamko hilo huku likiwataka viongozi kuzingatia haki za binadamu kama zilivyoainishwa kwenye katiba.
0 comments:
Post a Comment