Hii inaweza ikawa sababu nyingine ya mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona Lionel Messi kutajwa katika list ya mchezaji bora wa muda wote kama ambavyo Diego Maradona na Pele wanatajwa, nimekutana na hii mtandaoni mtu wangu nikaona ni bora nikusogezee.
Huenda ikawa inachekesha lakini ndio ukweli ambao wengi wetu hatujui, klabu ya Chelsea ilianzishwa mwaka 1905, hivyo ina miaka 110 toka kuaznishwa kwake, Chelsea ina jumla ya mataji 25 ambayo imewahi kutwaa. Miongoni mwa mataji ambayo Chelsea imetwaa ni pamoja na Ligi Kuu Uingereza na Klabu Bingwa Ulaya.
Kwa upande wa Lionel Messi yeye pekee ana mataji mengi zaidi ya klabu ya Chelsea, Stori kutoka www.ca2015.com Lionel Messi ambaye ana umri wa miaka 28 amefanikiwa kutwaa mataji 26. Miongoni mwa mataji aliyotwaa Lionel Messi ni pamoja na mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Laliga, Klabu Bingwa Dunia. Hii inamfanya Messi kuwa na umri mdogo lakini ana mataji mengi kuliko Chelsea.
0 comments:
Post a Comment