Mgombea
Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Arusha
Mjini, Mh Godblees Lema ameibuka Mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa
Jimbo hilo.
Katika
uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya Siasa Mh Lema amepata kura
68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa sawa na asilimia 65.9
akifuatiwa na Mgombea wa CCM Bw Philemon Mollel aliyepata kura 35.907
sawa na asilimia 34.4.
Wagombea
wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Pamoja na Navo Mollel wa
ACT Maendeleo aliyepata Kura 342 sawa na asilimia 03, Zuberi Mwinyi wa
CUF aliyepata kura 106. Sawa na asilimia 0.1, na Makama Rashidi wa NRA
aliyepata kura 43 sawa na asilimia 0.04.
Kwa
mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Bw Juma Iddy, jimbo la
Arusha wapiga kura walioandikishwa ni 317.814, na waliojtokeza kupiga
kura ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 na kura halali ni 104,353.
0 comments:
Post a Comment