VIONGOZI WA KIDINI KENYA KUONGOZA MAOMBI YA KITAIFA JUMANNE
Laranja amewataka wakenya kuonyesha umoja na nguvu kwa pamoja licha ya hayo ambayo yametokea katika jengo la biashara la Wastegate ambalo watu zaidi ya 60 wameripotiwa kufariki dunia wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya baada ya watu zaidi ya 10 ambao inaaminika ni wanachama wa kundi la kigaidi la Al Shabaab kuvamia jengo hilo mchana wa jumamosi iliyopita.
Aidha pia viongozi mbalimbali wa nchi hiyo akiwemo aliyekuwa waizir mkuu wa kwanza wa nchi hiyo cheo ambacho hakipo tena kwa wakati huu mheshimiwa Raila Odinga amekaririwa akisema kuwa magaidi wasiwagawe wakenya bali waendelee kuonyesha umoja wao na kumalizia kwakusema kwamba fikra na maombi yake yafike kwa f amilia zote zilizopoteza ndugu zao katika tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment