Home »
» DEREVA BODABODA IRINGA ATEKWA NA KUUAWA NA WATU WASIOJULIKANA
|
IRINGA
Zikiwa zimepita siku chache toka mmoja kati ya
madereva boda boda mjini Iringa kutekwa kisha kujeruhiwa vibaya kablaya
kuporwa pikipiki yake ,unyama huo dhidi ya madereva boda
boda umeendelea kutikisa mji wa Iringa baada Kijana mmoja mkazi wa
kihodombi kutekwa kisha kuuwawa kinyama.
Tukio hilo la kinyama limetokea usiku wa leo baada
ya kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Edger Lalika kukutwa
ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani .
Mashuhuda wa tukio hilo
wamesema kuwa tukio la
kuuwawa kwa dereva boda boda huyo liletokea eneo
la Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Hata hivyo kijana huyo anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka
25,ameuwa akiwa anafanya shughuli zake za bodaboda baada ya
kukodiwa na mteja wake huyo ambae aliamua kuitoa roho yake kabla ya
kumpokonya boda boda.
Kutokana na tukio hilo baadhi ya madereva bodaboda wamelaani
vikali kitendo hicho na kuwataka madereva bodaboda wengine kuungana na
kushirikiana na jeshi la polisi kufichua vitendo hivyo vya utekaji na
mauwaji dhidi ya madereva boda boda.
akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani
iringa bw ramadhan mungi amelaani vikali kutokea kwa mauaji hayo na kuiomba
jamii kutoa ushirikiano wa kutosha ili kumbaini mhusika
| | | | |
0 comments:
Post a Comment