MAKALA: CECILE KYENGE, TOKA CHINI KWENDA JUU, KUTOKATA TAMAA KWAMTOA
Dakta Cecile Kyenge katika mojawapo ya mikutano. ©Reuters |
Nilipokuwa mtoto, na nikakosea kisha mama aniseme, nilitamani anipige tu
mambo yaishe – unajua ni namna gani maneno yanachoma. Ndio maana hata
kuna utani kwamba mzaramo anaweza kukusema hadi ukafa. Haya yote ndio
yananirejesha kwa Cecile Kyenge, mwanamama wa kwanza kuwa waziri mweusi
nchini Italia.
Kila nikimtazama mama huyu mzawa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Napata ahueni – ahueni kwamba hata kama watu wakikupiga kwa maneno, bado
unaweza kutekeleza yale uliyonuia kufanya bila chembe ya wasiwasi.
Wanaomsema wanatokea kila upande – kuanzia viongozi wenzake, hadi
wananchi ambao anawatumikia. Ugumu anaokutana nao, unaweza pia
kulinganishwa na ugumu anaoupata mchezaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo,
Mario Ballotelli – ambapo amewahi kuzungumzai historia yake ya kukachwa
na wazazi wake akiwa mdogo, na kuasiliwa na familia mojawapo ya
wataliano kabla hajawa raia na hatimaye kulitumikia taifa lake jipya
kupitia timu ya taifa, akisakamwa na maneno lukuki kuanzia ndani hadi
nje ya uwanja.
Balotelli bado ni kijana, na kwa utukutu wake, ameshatoa majibu mengi
ikiwamo ya mkato na hata kuwa mkali zaidi pale anapochukizwa na hata
bosi wake.
Ninachokiona ndani ya huyu mama ndicho kinanivuta hasa kuandika hivi, na
tayari ninajifunza kitu kwake. Ni mvumilivu, asiyetetereka (japo
inavunja moyo sana) wala kushambulia wale ambao wanamtuhumu kwa mambo
mengi kwenye nafasi yake ya uwaziri anayeshughulikia uhamiaji.
Dakta Kyenge ofisini. ©Gregorio Borgia/AP |
Matukio;
Makamu wa Rais wa senate nchini humo ameshawahi kunukuliwa kisema kuwa
anapenda wanyama, na kila akimuangalia Cecile haoni tofauti na nyani
aina ya Orangutan. Kauli hiyo ya kiongozi wa juu ilijibiwa kwa ufupi na
Bi Kyenge ya kwamba, kama kiongozi huyo ameshindwa kuitumikia nafasi
yake, ni vyema basi akaachia kiti.
0 comments:
Post a Comment