MAKUMI ELFU WAJITOKEZA KUIOMBEA SYRIA AMANI
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kwenye maombi ya kufunga ya masaa manne kwa ajili ya taifa la Syria. ©AP |
Makumi elfu ya watu walijitokeza siku ya Jumamosi katika kuitikia wito wa Papa Francis,
ili kuombea amani taifa la Syria, ambalo limekuwA katika vita ya
wenyewe kwa wenyewe, ambapo na kwa sasa Marekani wanataka kushambulia
taifa hilo kutokana na kusadikika kutumia silaha za sumu huko Damascus
mnamo Agosti 21.
Papa Francis alitumia wasaha huo kuomba kimya kimya, ambapo wananchi
waliojitokeza kwenye uwanja wa Mtakatifu Petro walibeba bendera za Syria
pamoja na vipeperushi vilivyosomeka, "Achaneni na Syria", mengine
yakisomeka, "Msiishambulie Syria".
Maombi haya yaliyotangazwa na Papa tarehe mosi Septemba, yaliitikiwa na
maaskofu maeneo mbalimbali kuanzia Italy, Cuba, na sehemu nyinginezo,
ambapo pia huko Damascus, mufti mkuu alimshukuru Papa kwa jitihada zake
na kuwaalika waislamu kufunga na kuomba kwa pamoja na wenzao walioko
Roma.
Papa Francis akiendelea kusali kwenye mfungo huo wa wa kuiombea Syria. ©AP |
"Wahindu, Wabuddha, na hata wasio na dini wote walijitokeza kufunga kwa ajili ya suala hilo. haya ni mafanikio makubwa sana". Anasema mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Anata.
0 comments:
Post a Comment