MASANJA MKANDAMIZAJI YUKO MAREKANI KUHUBIRI
Masanja alipokuwa jijini New York alipokwenda kwa mara ya kwanza. |
Masanja amemshukuru Mungu kwa nafasi anayoipata hasa ikizingatiwa kwamba hii ni mara yake ya pili ambapo amekiri kuwa Yesu ndiye anafanya yote haya katika maisha yake kwakuwa hajawahi kufikiria kwamba siku moja atakanyaga Marekani maana tangu ameanza kazi ya uchekeshaji hajawahi kufika huko ila alipompokea Yesu anaona milango ikifunguka zaidi na zaidi. Masanja akiwa huko akimaliza kilichompeleka amepanga kurekodi baadhi ya vipande vya vipindi vya Original Comedy ambavyo itakuwa kuwafundisha watanzania na vijana nini watu wa Marekani wanafanya.
Aidha katika mahojiano na Silas Mbise kupitia kipindi cha Gospel Celebration cha WAPO Radio Fm mda mchache uliopita mwigizaji huyo atakuwa nchini Marekani kwakipindi cha mwezi mmoja amemtaka mtangazaji huyo kuoa maana kuchelewa kwake kunafanya wengine kuchelewa mwe mwe mwe Silas si akajikausha ha ha ha, kijana akaishia kukata simu na kusema wakati wa Bwana ukifika atafanya hivyo. Ila kweli anatuchelewesha kha!
0 comments:
Post a Comment