HATIMAYE MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA KENYA EMMY KOSGEI AFUNGA NDOA NA MCHUNGAJI WA NIGERIA, ANGALIA PICHA ZOTE
Emmy na mumewe mwenye tai ya zambarau mchungaji Anselm Madubuko mara baada ya ndoa yao. |
Awali kabla ya ndoa hiyo kumekuwepo maneno mengi kwanini mwimbaji huyo ameamua kuolewa na mchungaji huyo na wengine wakitoa na majibu kabisa kwamba amefuata pesa za mchungaji huyo bali wanapendana na kuwataka watu hao kuacha kufuatilia mambo yake na mahusiano na mumewe huyo, ambapo hakuacha kuweka bayana kwamba amekuwa akipendwa na kupewa matunzo kama malikia na mumewe huyo ambaye naye kwa upande wake amekaririwa akisema kwamba anampenda mwimbaji huyo pia uamuzi wa kumuoa alipewa ruhusa na mwanae mwenye miaka 25 aliyempata na mkewe Connie aliyefariki dunia mwaka jana, "hata kama ningesubiri kwa miaka zaidi bado haitasaidia kumsahau mke wangu, hata miaka 20 haitoshi bado, nimeamua kusahau na kusonga mbele ndio maana nimeamua kuoa sasa kipindi kifupi toka mke wangu afariki dunia" amesema mchungaji Anselm
Aidha mchungaji huyo ameongeza kuwa " nilioana na mke wangu na kuishi naye kwa miaka mingi lakini ghafla ameniacha pekee, mambo mengi yamepita, nimechagua kusikiliza akili na Mungu wangu ananiambia nini, amenichagulia Emmy inatosha kwasasa naangalia mbele zaidi kuongeza familia yangu kwakuwa na watoto na mke wangu mpya" alisema mchungaji Anselm akizungumza na jarida la Encomium.
Harusi ya kitamaduni ilifanyika siku ya alhamisi iliyopita wilayani Koibatek kijijini kwakina Emmy maeneo ya Kelelwa karibu na barabara kubwa ya Ravine, ambapo harusi kubwa inatarajiwa kufanyika huko Nigeria mapema wiki ijayo. Mungu abariki ndoa yao.
0 comments:
Post a Comment