Mbunge wa viti maalumu ccm wa mkoa wa iringa mh; Rita Kabati amewaasa wanawake kote nchini kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali pindi muda wa kuchukua form utakapo fika.
Akizingumza na nuru fm katika kipindi cha sun rise power amesema wanawake wote lazima watambue kuwa wanaweza bila kuwezeshwa hivyo wasijidharau kuchukua form na kujitokeza kuchukua form kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu.
Aidha amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanawake wanapata elimu ameandaa semina mbalimbali kwa ajili ya ya kuwaelimisha wanawake juu ya katiba inayopendekezwa ili muda ukifika wa kuipigia kura waweze kuipigia katiba hiyo.
Hata hivyo amewaomba wanainchi kuzisoma na kuzipokea katiba zinazopendekezwa na kuzielewa ili kuweza kuzipigia kura .
0 comments:
Post a Comment