WATUHUMIWA WANNE WA UHALIFU WA TANGA WAKAMATWA,WAMO WASOMALI NA WENYE ASILI YA KIARABU.
Watuhumiwa
wanne wa makundi ya uhalifu waliokuwa wamejificha katika mapango ya
maji moto eneo la Amboni jijini Tanga, wametiwa mbaroni na jeshi la
polisi kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na wananchi wa kata ya Mzizima
ambao wameitikia wito wa jeshi hilo ili kuhakikisha wanaishi kwa
usalama.
Habari
zilizothibitishwa na viongozi wa jeshi la polisi ambao sio wasemaji,
baadhi ya watuhumiwa ni wenye asili tofauti wakiwemo wenye asili ya
Kiarabu huku wengine wakiwa na asili ya Kisomali ambao wote kwa pamoja
wamekamatwa na wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi hatua
iliyosababisha operesheni ya vyombo vya usalama kupunguza kasi tofauti
na ilivyokuwa siku nne zilizopita na kusababisha eneo la tukio kuwa
kimya kuashiria hali inaelekea kuwa shwari.
Baadhi
ya wananchi walioshiriki katika zoezi hilo wakielezea jinsi
walivyowadhibiti watuhumiwa ambao walikamatwa kwa nyakati tofauti wakiwa
wamechoka katika vichaka vilivyopo pembeni mwa mapango ya maji moto
yaliyokuwa yakihifadhi wahalifu yaliyopo kilomita 5 kutoka katika yale
mapango ya Amboni yaliyozoeleka ambayo yanamilikiwa kisheria na serikali
kwa ajili ya kukuza sekta ya utalii, wamesema kukaa na njaa ndio sababu
kuu iliyowafanya kuwakamata kiurahisi kisha kuwapigia simu askari wa
jeshi la wananchi kwa lengo la kuwakabidhi watuhumiwa.
Hata
hivyo jitihada za kumpata kamishna wa operesheni wa jeshi la polisi
nchini afande Paul Chagonja ili kutoa taarifa rasmi kuhusu sakata hilo
bado zinaendelea lakini awali amekiri kuwa jeshi hilo litawapa motisha
watu walioshirikia katika zoezi la kufichua wahalifu hatua ambayo
inasubiriwa na wasamaria wema.
0 comments:
Post a Comment