Huyu ndo Kiongozi wa Kikundi cha Kigaidi Kinachoua Polisi na Kuiba Silaha Kwenye Vituo Nchini.....Anaitwa Kaisi Bin Abdullah.
Hatimaye kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti la Ijumaa kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiita Kaisi Bin Abdullah akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!
Gazeti hilo linadai kuunasa mkanda huo
kutoka kwa mtu mmoja aliyekataa kujitambulisha kwa jina wala kusema
anakotokea hapa nchini.
Bin Abdullah ametumia dakika 11: 03 kuzungumzia mambo mbalimbali lakini kubwa kuliko yote ni kuliponda Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuwakamata wenzao katika imani na harakati (zinazohifadhiwa kwa sasa) na kuwashikilia kwenye mahabusu mbalimbali nchini.

Alianza kwa Kusema:
Bin Abullah ambaye kwenye mkanda huo amevaa nguo nyeusi kama ninja na
miwani ya giza, alizungumza kwa kirefu, akitoa wito lakini mbele
akasema:
“Tumeshaungana ili kupambana. Mkoa wa Mtwara zaidi ya wenzetu kumi na
saba walikamatwa kwa makosa ya dhuluma, makosa ya kupanga, makosa ya
ugaidi.
Ishirini na moja wamekamatwa Zanzibar wako katika Gereza la Segerea (Dar). Wenzetu wengine kumi na nane wamekamatwa Mwanza wako katika Gereza la Kisongo, Arusha. Ndugu zangu, wenzetu wengine kumi na saba wameuawa Mtwara kwa amri ya ...(anamtaja waziri).”

“Subira yetu imefika
mwisho na tulichokuwa tunasubiri Mungu ameshatupa. Tunatoa ahadi
kilichopo hivi sasa tunatoboa jahazi wote tuzame.
“Tunatoa rai, wenzetu waliopo Gereza la Kisongo waachiwe huru. Hapa hatumtishi mtu yeyote yule.”
“Pili, agizo la Ernest
Mangu IGP, umetangaza uliwenguni kwamba umewakamata wote waliovamia
vituo vya polisi na umezikamata silaha zote. Ukweli ni kwamba unatetea
tumbo lako. Hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa na wala silaha
hazijakamatwa.
“Mungu ametukubali. Katika Kituo cha Polisi Ushirombo (Kilimanjaro)
tumeweza kuvamia kituo, tukaweza kutoa roho za polisi na tukaweza
kuchukua silaha, tunazo.
“Tumevamia Kituo cha Polisi Ikwiriri (Pwani), tumeweza kuchukua silaha za kutosha, tumeweza kuchukua mabomu ya kutosha. Tunazo silaha tunasubiri muda zianze kufanya kazi.
“Tumevamia Kituo cha Polisi Ikwiriri (Pwani), tumeweza kuchukua silaha za kutosha, tumeweza kuchukua mabomu ya kutosha. Tunazo silaha tunasubiri muda zianze kufanya kazi.
“Ernest Mangu nakupa changamogto, hivi sasa tuna uwezo...(maneno yanahifadhiwa kwa usalama) wakati wowote ambao tunataka.
“Tumeweza kuchukua silaha bila
kuwa na silaha yoyote. Ndugu zetu wa Tanga wameweza kuchukua silaha
wakiwa hawana silaha yoyote. Ikwiriri tumechukua silaha tukiwa hatuna
silaha yoyote, mpaka sasa tumeshachukua roho tano za polisi.
“Ndugu zangu, ...mlikuwa
mkinisubiri nitoe tamko, natoa kauli rasmi...” alihitimisha Abdullah,
huku vitisho vya jumla kwenye tamko lake vikiwahusu polisi, viongozi wa
ngazi za juu serikalini pamoja na mikusanyiko ya ibada.
Tamko la IGP
Baada ya video hiyo,Gazeti la Ijumaa lilimtafuta Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu
na kuzungumza naye kuhusu mtu huyo na kumkabidhi video ambapo alisema:
“Nawashukuru sana kwa kuleta video hii, huu ndiyo ushirikiano
unaotakiwa, nawaomba wananchi video za aina hii wazikatae kwa sababu ni
kosa kuwa nazo na watu kadhaa wameshakamatwa kwa kuwa nazo.
“Sisi kama jeshi la polisi tunajua kuwa kuna watu wanadhani kufanya
uhalifu kama huo kutawasaidia kutimiza matakwa yao, lakini ukweli ni
kwamba polisi wapo imara na nina uhakika watuhumiwa watakamatwa kwa
kushirikiana na raia wema.”
Shehe Mkuu Amkana
Baada ya kuzungumza na IGP, Gazeti lilimtafuta Shehe Mkuu Tanzania, Mufti Shaban Simba na kumsimulia
kuhusu kuibuka kwa Bin Abullah na kutaka kujua pengine anamfahamu.
0 comments:
Post a Comment