Ashitakiwa kwa Kumtia Vidole Sehemu za Siri Mtoto wa Miaka Minne.
MKAZI wa Bangulo Hali ya Hewa, Baraka Benson (30) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, akikabiliwa na mashitaka ya kumnajisi mtoto wa miaka minne.
Benson alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Hassan Juma.
Wakili
wa Serikali, Florida Wenslaus alidai kwamba Desemba 23 mwaka jana,
maeneo ya Bangulo Hali ya Hewa Wilaya ya Ilala, Benson alimnajisi mtoto
huyo wa miaka minne kwa kumtia vidole sehemu za siri huku akijua kufanya
hivyo ni kosa kisheria.
Mshitakiwa
alikana mashitaka na kurudishwa rumande kwa kushindwa masharti ya
dhamana. Awali, wakili Wenslaus alidai kwamba upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa
maelezo ya awali.
Hakimu
Juma alimtaka mshitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja kutoka
taasisi inayotambulika, watakaosaini dhamana ya Sh milioni mbili.
0 comments:
Post a Comment