WATOTO WATATU WALIOUAWA NA KULIWA MIOYO YAO NA MAMA YAO WAZIKWA.
Moja
ya taarifa kutoka Nairobi Kenya ambayo ilisikitisha sana ni tukio la
watoto watatu kuuawa na mwanamke mmoja ambaye baada ya kuwaua halafu
akawapasua na kula mioyo ya watoto hao.
Mwanamke huyo Catherine Muthoni alimuua mtoto wake mmoja mwenye umri wa miaka kumi na baadaye kuua watoto hao wawili wa jirani.
Tukio
la leo katika eneo la makaburi ya Lang’ata limewatoa wengi machozi
wakikumbuka jinsi watoto hao walivyofariki kwa mateso ambapo familia ya
watoto hao wameamua kufanya mazishi ya watoto wote wawili kwenye kaburi
moja.
Mwanamke
huyo anashikiliwa na Polisi kesi yake ikiendelea ambapo Mahakama
iliagiza afanyiwe uchunguzi kama ana matatizo ya akili huku upelelezi wa
kesi yake ukiendelea.
Hapa iko taarifa hiyo kwenye video kutoka K24 TV Kenya..
0 comments:
Post a Comment