MAKUBWA..!! MTOTO AUA BABA YAKE MZAZI KWA KUMPIGA NA KOLEO KICHWANI KISA WIZI HUKO TARIME.
Vilevile
inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alijeruhiwa kwa kucharangwa kwa panga na
baba yake huyo kabla ya kumjeruhi kwa kumpiga na koleo kichwani na
ubavuni baada ya kuzuka ugomvi baina yao.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Forodhani Sirari, Nyangoko Paulo alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo Ijumaa ya wiki iliyopita jioni katika kitongoji hicho.
Paulo alisema kuwa ugomvi huo uliibuka baada ya baba kumtuhumu mwanaye kuwa anatabia ya wizi.
Alisema
inadaiwa kuwa baba huyo alimweleza mwanaye huyo kuwa aliwahi kufanya
wizi kitendo kilichosababisha kutozwa faini ya ng'ombe.
Paulo alisema inadaiwa kuwa baada ya baba kutoa tuhuma hizo, mwanaye alitoroka na kuwa nje ya familia kwa zaidi ya miaka mitano.
Alisema
aliporudi nyumbani kwao, baba alikerwa na kuanza kumfukuza kwa panga
ili asiingie ndani kwake huku akisisitiza aende akaishi kwa wahalifu
wenzake.
Mwenyekiti alisema baba akirusha panga na kumkata mkononi, mwanawe alichukua koleo na kumpiga nalo kichwani na ubavuni.
Alisema
majirani walijitokeza kumuokoa na kuwakimbiza Hospitali ya Wilaya
Tarime ambako alikufa kabla ya kuanza kupatiwa matibabu.
0 comments:
Post a Comment