Kibiki akibadilishana mawazo na mmoja wa wanachama wa tujiwezeshe cha kituo kikuu cha mabasi mjini Iringa
Katibu wa kikundi cha tujiwezeshe chenye wanachama zaidi ya 560, wa
kituo kikuu cha mabasi mjini Iringa Manet Charles akizungumza baada ya
kumkabidhi sh 110,000 mwanachama mwenzao Frank Kibiki, ambaye ni
mwanahabari baada ya kutangaza nia wa kuomba kuwania ubunge wa jimbo la
Iringa mjini kupitia CCM.
Kibiki mwenye koti jeusi,
akiwashukuru viongozi wa tujiwezeshe kwa msaada huo, na kuomba wavumilie
muda ufike kwani fedha hiyo ataitunza
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
NYOTA ya mwandishi wa Habari wa gazeti la Uhuru, Frank
Kibiki ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la
Iringa mjini, endapo chama chake cha CCM kitampitisha imeendelea kuwaka baada
ya vijana wa stendi kuu ya mabasi mjini Iringa, kumchangia fedha, kwa ajili ya kuchukulia
fomu wakati ukifika.
Vijana
hao wamesema wameamua kuchangishana fedha ili kufanikisha zoezi la Mwandishi
huyo kuchukua fomu, wakiamini ni mwenzao.
Kibiki amechangiwa
fedha hizo, ikiwa ni siku chache tu zimepita, tangu wasanii wa muziki wa kizazi
kipya manispaa ya Iringa wakiongozwa na ‘One lee’kumkabidhi zawadi ya wimbo
ambao, tayari umeanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio mjini humo.
Kiongozi
wa vijana hao, Maneti Charles alisema ni wakati wa kijana wa kawaida, kutoka
miongoni mwao kuongoza jimbo la Iringa mjini na kuitaka CCM manispaa ya Iringa,
ihakikishe inampitisha mtu anayekubalika kwa jamii.
Amesema mpaka sasa wamefikisha kiasi cha Sh 110,000 ambazo wamemkabidhi wakitaka azitunze mpaka wakati wa kuchukua fomu ukifika.
“Kibiki
ni mwenzetu, siku zote tumekuwa tukishinda naye na tunaujua uwezo wake,
tumechangishana fedha mwenye mia moja, miambili, miatano ili tumsaidia wakati
ukifika tumchukulie fomu.” Alisema.
Tangu
kutangaza nia, Kibiki ambaye ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM taifa, na Katibu
mwandamizi wa UVCCM kwa miaka zaidi ya miaka 10, anadaiwa kuharibu upepo wa vigogo
wa chama hicho ambao walikuwa wakitajwa kunyemelea jimbo la Iringa mjini.
Vijana
hao, wamemtaka Kibiki kutoogopa wala kukata tamaa badala yake, wao watamsemea
mahali popote wakidai kuwa sifa kuu ya kiongozi ni kukubalika kwa watu wa riza
zote na kushirikiana na wananchi bila kujali matabaka yao.
“Tunamkubali
kaka, wala asiogope sisi ndio tutakuwa mbele yake, tunachotaka ubunge urejee
kwetu sisi wana Iringa wenye ubunge kwani huu ni utumishi ambao sisi ndio
tunaowatuma hawa wabunge,”alisema Enos Mgala, muuza pipi wa kituo cha mabasi,
Iringa mjini.
Jimbo
la Iringa mjini ni mionngoni mwa majimbo yenye upinzani mkali, tangu Mbunge wa
jimbo hilo,
Mchungaji Peter Msigwa(chadema), alipolipokonya kutoka kwa wapinzani wake chama cha mapinduzi (CCM).
Kila raheli wanahabari..
ReplyDelete