MGANGA WA KIENYEJI AKAMATWA NA BUNDUKI ILIYOTUMIKA MAUAJI YA MWANAMKE MJINI KAHAMA NA UJAMBAZI.
Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia mganga wa kienyeji Zacharia
Ngobeko Dogo(35),mkazi wa kijiji cha Mbulu kata ya Mhongolo wilayani
Kahama kwa kosa la kukutwa na bunduki aina ya SMG yenye namba 8945
iliyotumika katika mauaji ya Mary Kashindye aliyeuawa kwa kupigwa
risasi hivi karibuni wilayani Kahama.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha(Pichani) amesema
mganga huyo wa kienyeji alikamatwa akiwa na silaha hiyo ikiwa na risasi
nane ndani ya magazine iliyokuwa imehifadhiwa nyumbani kwake tarehe
18,2015 saa saba mchana.
Kamanda
Kamugisha amesema mganga huyo na wenzake wawili wanatuhumiwa kuhusika
katika matukio ya mauaji yaliyotokea tarehe 8 mwezi huu saa tatu usiku
kwa kumuua Mary Kashindye kwa kumpiga risasi kutokana na ugomvi wa
kiwanja kati ya marehemu na Jumanne Maige.
Amesema
kutokana na ugomvi huo aliwakodi Andrew Buteye Mtakatifu(38) mkazi wa
Tabora na Daudi Luchemela Ngasa(40) mkazi wa Nzega Tabora kutekeleza
mauaji hayo.
Ameongeza
kuwa silaha hiyo pia ilitumika katika unyang’anyi wa kutumia silaha wa
tarehe 13 mwezi huu saa mbili usiku wilayani Kahama ambapo walipora
shilingi milioni moja na nusu dukani kwa Manyangu Mboje.
Kamanda
Kamugisha ameeleza kuwa katika mahojiano na watuhumiwa,wamekiri
kuhusika katika matukio yote mawili na kuhifadhi silaha kwa mganga huyo
wa kienyeji.
Katika
hatua nyingine amesema watuhumiwa wamekiri kutenda makosa ya
unyang’anyi kwa kutumia silaha katika mkoa wa Mbeya,Mwanza na Tabora.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
0 comments:
Post a Comment