WATU WATATU WAFARIKI DUNIA KWA KUTEKETEA KWA MOTO KWENYE GARI.

Watu
watatu wamefariki dunia kwa kuungua moto hadi kuteketea kabisa akiwemo
dereva na utingo wake baada ya lori la mafuta kuacha njia na kupinduka
na kuungua moto katika eneo la Maseyu barabara ya Morogoro Dar es
Salaam.

Kikosi
cha zimamoto walichukua muda kuuzima moto huo kutokana na kusambaa
ambapo hata hivyo hakukua na matukio ya watu kujitokeza kuiba mafuta
kama ilivyozoeleka.
Baada
ya kumaliza kuuzima moto huo kikosi cha zimamoto na uokoaji wakafanya
juhudi nyingine za kuvuta kwa craine na kukata kwa kutumia mashoka
mabaki ya lori hilo baada ya walioshuhudia tukio hilo kueleza kuwa watu
wote waliokuwemo katika gari hawakutoka ambapo baada ya muda miili
mitatu iliokolewa ikiwa imeungua kabisa.

Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo madereva wa malori ambapo
walikuwa wakisafirisha mafuta katika kampuni moja Farhan Yusufu amesema
lori hilo lilikua limesheheni mafuta ya Dezel mali ya kampuni ya Petrol
Africa ilikua ikitokea Dar es salaam kwenda jijini Mwanza ambapo
ilipoteza uelekeo na kupinduka kisha kuwaka moto.

Waliofariki
dunia ni Ahmed Dilie dereva na utingo wake aliyefahamika kwa majina ya
Emela na mtu mmoja ambaye bado hajaweza kufahamika mara moja.
0 comments:
Post a Comment