KUMBE MAITI ZA WATOTO WALIOKUFA ZINAUZWA KWA WAGANGA WA KIENYEJI HUKO SIMIYU..!! WAUGUZI NA MADAKTARI WATAJWA

Wakati
serikali ikihaha kutafuta muarobaini wa mauaji ya watu wenye ulemavu
Ngozo (Albino),katika mikoa ya kanda ya ziwa,huku ikidiriki kutangaza
vita dhidi ya wapiga ramli wote, katika hali isiyokuwa ya kawaida
imebainika kuwa watoto ambao huzaliwa wakiwa hawajafikisha umri na kufa
au kupoteza maisha wakati wa kuzaliwa viungo vyao huuzwa kwa waganga wa
kienyeji katika hospitali ya wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.
Inaelezwa
kuwa akina mama wanaojifungua watoto hao na kwa bahati mbaya kupoteza
maisha, viungo vya watoto hao huwa havipelekwi kuzikwa kama ilivyo
kawaida na taratibu za hospitali, badala yake wauguzi na wafanyakazi
wengine huchukua viungo hivyo na kupeleka kwa waganga wa jadi.
Tuhuma
hizo zilitolewa juzi mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Mwamvua
Jilumbi katika kikao cha pamoja na wadau wa afya mkoa kilichofanyika
katika ukumbi wa kanisa la KKKT mjini Bariadi wakati wa uzinduzi wa
mpango mkakati wa kukomesha vifo vya wajawazito
na watoto mkoani Simiyu ulioko chini ya AMREF Tanzania.
na watoto mkoani Simiyu ulioko chini ya AMREF Tanzania.
Wadau
hao walibainisha kuwa hali hiyo imekuwa ikijitokeza kila mara katika
hospitali ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo walieleza kuwa
mtandao mzima wa kuuzwa kwa viungo hivyo ufanyika kati ya wauguzi pamoja
na madaktari ambao ndiyo wahusika wakuu kuzalisha akina mama
wajawazito.
Mbele
ya Katibu huyo tawala wa Mkoa wadau hao waliendelea kueleza kuwa viungo
hivyo vimekuwa vikiuzwa kuanzia shilingi 400,000 hadi 500,000 kiasi
ambacho walieleza hutolewa na waganga wa hao wa jadi.
“..katika
hospitali yetu ya Bariadi kuna jambo ambalo siyo zuri na jema leo ngoja
tulitoboe mbele ya kikao hiki na tena mbele za waandishi wa habari na
wewe Katibu tawala wa Mkoa..akina mama wanaojifungua watoto wao kwa
bahati mbaya akafariki viungo vya watoto hao huuzwa kwa waganga wa jadi”
Alisema Gasper Mathew na kuongeza kuwa..
“
viungo hivyo vinauzwa shilingi 400,000 hadi 500,000 huu ni ushirikina
wa hali ya juu na ni hatari..wauguzi pamoja na madaktari ndiyo
wanahusika sana..wamekuwa wakipewa kiasi hicho..kila mara wanafaya hivyo
lakini tumekuwa kimya” Alisema
Walisema
kuwa akinamama wengi hufika hospitalini hapo kwa lengo la kujifungua
na mara wanapojifungua na kwa bahati mbaya mtoto au watoto kufariki
kutokana na matatizo ya afya ya uzazi baadhi huamua kuwahifadhi katika
chumba cha maiti lakini wengi hujikuta wakirejea nyumbani mikono mitupu
baada ya miili ya watoto wao kuuzwa kwa waganga wa kienyeji.
Akizungumzia tuhuma hizo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,Mwamvua
Jilumbi katika kikao hicho alimtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Bariadi Erica Mssika kutoa maelezo juu ya tuhuma hizo.
Jilumbi katika kikao hicho alimtaka Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji wa Bariadi Erica Mssika kutoa maelezo juu ya tuhuma hizo.
Akitoa
maelezo ya tuhuma hiyo Mkurugenzi huyo alisema kuwa hana taarifa yoyote
juu ya kuwepo kwa vitendo hivyo katika hospitali yake, huku akieleza
kuwa watafanya uchunguzi mara moja na watakao bainika kufanya hivyo
watachukuliwa sheria mara moja.
“..hii
ni hatari mimi hili nimelipata hapa na nimelisikia leo sina taarifa
yeyote.. ila nawaomba wadau waliotoa tuhuma hizi tushirikiane tufanye
uchunguzi haraka ili tuwabaini na watakaobainika tutawachulia sheria za
kinidhamu” Alisema Mssika.
Katika
kikao hicho Meneja Mradi wa Shirika lisilo la kiserikali
linalojihusisha na masula ya afya AMREF Health Africa tawi la
Tanzania,katika mkoa wa Simiyu, Godfrey Matumu, aliitaka jamii ya mkoa
wa Simiyu kushiriki kikamilifu katika kuthibiti vifo vya akinamama
wajawazito na watoto wachanga wenye umri chini ya miaka mitano.
0 comments:
Post a Comment