MASIKINI KIJANA HUYU!!!!!!AINGIZWA MOCHWARI AKIDHANIWA AMEKUFA.
Kijana mmoja, Omary Ramadhani, 28, mkazi wa Sinza Madukani, Dar
amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya kugongwa na ‘Break Down’
alipokuwa akiendesha Bajaj katika makutano ya Barabara ya Sam Nujoma na
Ali Hassan Mwinyi, Mwenge, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa masikitiko, Omary alisema kuwa alipogongwa na gari hilo
hakuweza kujitambua kwani hata wasamaria wema walivyomchukua na
kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walijua alifariki
dunia hivyo wakamuingiza moja kwa moja mochwari, lakini kwa bahati nzuri
alitokea nesi mmoja aliyeshauri asiwekwe kwanza kwenye friji mpaka
apimwe.
Akiendelea kuzungumza kwa tabu kutokana na maumivu ambayo anayo, Omary
alisema baada ya nesi huyo kumpima aligundua alikuwa akipumua kwa shida.
Alisema hata ndugu zake walijua ameshafariki dunia kutokana na
alivyokuwa, kwani alivunjika mgongo mara sita na mfupa wa mkono ulitoka
nje na kupasuka kichwani jambo lililosababisha kuvuja damu nyingi.
Alifafanua kuwa kutokana na hali yake, alikimbizwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi ambapo baada ya siku tatu alizinduka na walipokuja
ndugu zake aliwauliza alikuwa wapi, walipomuambia Muhimbili alizimia
tena.
Alisema
alipata matibabu kwa muda wa miezi sita ndipo aliruhusiwa kuondoka
lakini alitakiwa atoe shilingi 1,000,000 kwa ajili ya tiba maalum
kwenye mashine ambayo siijui jina, lakini nimeshindwa kuzipata na ndugu
zangu ni walalahoi.
Omary
alisema hivi sasa bado ana matatizo, haja ndogo haitoki sawasawa na
akienda maliwatoni huchukua zaidi ya saa moja kwani mkojo hutoka
kidogokidogo na kumsababishia maumivu makali ambapo haja kubwa anapata
mara moja kwa wiki.
Omary amewaomba Watanzania wenye moyo wa huruma kumchangia ili atibiwe, aepukane na mateso makali anayopata. Namba yake ni 0656 168 034.
0 comments:
Post a Comment