SASA WANAFUNZI KUFUNDISHWA SOMO LA NGONO SHULENI, WABUNGE NAO WABARIKI.
Shule
zote za serikali zikiwemo za msingi na zile za upili nchini Uingereza
zitalazimika kufunza somo la ngono na uhusiano SRE ,wabunge wa taifa
hilo wamesema katika ripoti yao.
Kamati
ya elimu katika bunge la Uingereza ilianzisha uchunguzi baada ya
kubainika kuwa zaidi ya theluthi moja ya shule zilikuwa zikishindwa
kutoa mafunzo ya somo hilo kwa umri unaohitajika.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Graham Sturat amesema kuwa vijana wadogo wana haki ya kupata habari ambazo zitahakikisha usalama wao.
Serikali imesema kuwa itaangazia matokeo ya ripoti hiyo.
Mwaka
2013 ripoti ya bunge hilo ilisema kuwa masomo ya kibinafsi,ya kijamii
,afya na elimu ya kiuchumi ambapo somo hilo la ngono limehusishwa
yanahitaji kuimarika katika asilimia 40 ya shule.
Wabunge
hao wamesema:Hali hii haitakubalika katika masomo mengine licha ya kuwa
harakati za serikali kuimarisha masomo hayo ni za kiwango cha chini.
Je,unakubaliana na wazo la bunge la Uingereza kuwafunza watoto wa shule za msingi somo la ngono na uhusiano?
0 comments:
Post a Comment