WATU WATATU WAUAWA KWA KUCHARANGWA SIME NA MAPANGA MAPIGANO YA WAFUGAJI NA WAKULIMA HUKO MOROGORO.
Watu
watatu wamefariki dunia wakiwemo wakulima wawili na mfugaji mmoja na
watu sita wamejeruhiwa vibaya kwa kukatwa kwa sime na mapanga kufuatia
mapigano yaliozuka kati ya wakulima na wafugaji katika mbonde la
matembele linaunganisha kijiji cha mabwegere na mbigiri wilayani kilosa
mkoani Morogoro.
Mkuu
wa wilaya ya kilosa Bw Elis Tarimo akizungumzia tukio wakati
alipotembelea majeruhi katika hospitali ya mission St Joseph dumila
amesema chanzo cha tukio hilo ni wafugaji wawili waliwahoji wakulima
waliokua katika shughuli za kutayarisha mashamba kuwa kwanini
hawajafuata taratibu za kujisajili na kuomba kibali kutoka serikali ya
kijiji.
Kufuatia
hali hiyo wakulima waliwajibu kuwa wameruhusiwa na mkuu wa mkoa walime
ndipo wakatoa taarifa kwa kundi la wafugaji wapatao 60 ambapo yakaanza
mapigano kwa kutumia mikuki marungu na sime na mapanga amewataja
waliofariki dunia kuwa ni Joseph Peter (26) mkulima ,Rajabu Selemani
(55) mkulima na Kaduru Kashu (30) mfugaji na wengine wamelazwa katika
hospitali na mmoja amehamishiwa katika hospital ya mkoa wa Morogoro.
Kufuatia
tukio hilo mkuu wa wilaya yakilosa Bw Elias Tarimo amesema tukio hilo
la mauji halita vumilika na lazima vyombo vya sheria vifanye kazi na
kuhakikisha watuhumiwa wanakamtwa huku akitupia lawama wizara ya ardhi
nyumba na maendeleo ya makazi kuchelewa kuleta wasuluhishi wa mgogoro
huo kama walivyoahidi ili kuhakiki upya mipaka ya vijiji ili kuondoa
migogoro ya wakulima na wafugaji iliyodumu kwa muda mrefu.
Nao
majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mission St Joseph Dumila
wamelalamikia serikali kushindwa kumaliza tatizo la migogoro ya wakulima
na wafugaji ambapo wameelezea mapigano yalivyotokea.
Naye
muuguzi wa zamu katika hospitali ya mission St Joseph Melania Shayo
amesema wakulima wawili waliofariki dunia wakati wakipatiwa matibu na
kukiri kupokea maiti moja ya mfugaji alieuwawa wakati wa mapigano hayo.
Mapigano
haya yamekuja siku chache ambapo nyumba 41 zilichomwa moto zikiwemo za
wakulima na wafugaji kufutia mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Mabwegre
wilayani kilosa ambapo mkuu wa wilaya aliwakutanisha wakulima na
wafugaji kwa lengo la kumaliza mgogoro huo ambapo hata hivyo mkutano huo
uligubigwa na mivutano na wafugaji na kuondoka kabla ya mkutano
kumalizika.
via>>ITV
0 comments:
Post a Comment