ALICHOKIJIBU MBUNGE MBATIA KUHUSU ISHU YA KUSEMA KUWA MREMA NI MGONJWA.
Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) alitoa hoja binafsi Bungeni kwamba MbungeJames Mbatia amekuwa akipita Jimbo la Vunjo na kuwaambia wapigakura wasimchague Mrema kwa sababu ni mgonjwa.
“Napenda kusema kuwa mimi ni mbunge halali wa Vunjo na Mbatia hatapata jimbo hilo na ninatangaza kuwa nitagombea tena na hafi mtu hapa“– Alisema Mrema wakati akimalizia kuwasilisha hoja yake hiyo.
Leo wakati wa kikao cha Bunge jioni, Mbunge Mbatia alipata nafasi kujibu kuhusu ishu hiyo; “Maelezo haya nayatoa kukanusha kwa moyo wangu wote matamshi yaliyotolewa ndani ya Bunge hili na Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema, Mbunge wa Vunjo. Siku ya tarehe 05/02/2015 wakati wa kuahirisha Bunge Mheshimiwa Mrema alitoa maelezo ambayo sio sahihi alipoeleza kuwa mimi James Francis Mbatia niliwahi kusema kuwa yeye ni mgonjwa anayeugua maradhi ya ukosefu wa kinga mwilini yaani UKIMWI“
“Maelezo
yote aliyoyatoa sio sahihi na sijawahi na sitawahi kutamka maneno
hayo… Sijawahi kumnyanyapaa Mheshimiwa Mrema wala mtu yoyote
aliyeathirika na maradhi ya aina yoyote“
“Mimi sina uadui na mtu yoyote akiwepo mheshimiwa Mrema hata
sasa hivi amekaa kwenye kiti changu sina ugomvi nae. Nimezaliwa na
nimekuzwa kwenye familia ya wacha Mungu siwezi nikafanya hivyo.. To
grow old is mandatory but to be wise is optional…”
“Mwaka
huu ni mwaka wa uchaguzi Mkuu ni rai yangu kwa watanzania wote wachague
vionzozi wenye uwezo, wacha Mungu, wakweli na wenye kuchukia
propaganda, ubaguzi, chuki, ubinafsi na ubinafsi“
“Baadhi
ya viongozi wanadai kuwa wana hatimiliki ya maeneo wanayoongoza dhana
hii sio sahihi, nataka kuwahakikishia Watanzania wenye hatimiliki ya
nchi yao ni Watanzania wenyewe“
0 comments:
Post a Comment