Rais Kikwete aongoza maziko ya Chifu Abdul Mkwawa ambapo Mwanafunzi wa Miaka 13 Ametawazwa kuwa Chifu Mpya wa Wahehe, akirithi nafasi ya baba yake
Mwanafunzi wa Darasa la Saba, Adam Abdul Sapi (13) ametawazwa kuwa Chifu mpya wa Wahehe, akirithi nafasi ya baba yake, aliyefariki na kuzikwa mkoani Iringa.
Rais
Jakaya Kikwete alishiriki maziko ya Chifu huyo wa Wahehe, Abdul Sapi
Mkwawa (66) yaliyokwenda sanjari na hafla ya kumsimika mtoto huyo
kushika wadhifa huo wa kimila.
Maziko
ya kiongozi huyo aliyefariki Februari 14, mwaka huu, yalifanyika
katika kijiji cha Kalenga, nje kidogo ya mji wa Iringa ndani ya
makumbusho yaliyowekwa fuvu la babu yake,Chifu Mkwavinyika Munyigumba
Mwamuyinga Mkwawa.
Mbali
na Rais Kikwete, wengine waliohudhuria maziko hayo ambayo taratibu zake
zilitumia takribani saa 2.30 kuanzia saa 7 mchana ni pamoja na Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Tanzania Bara,
Phillip Mangulla, wakuu wa mikoa ya Iringa na Mbeya na viongozi
mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa.
Kabla
ya kifo chake kilichosababishwa na maradhi ya sukari na figo, Abdul
Sapi Mkwawa aliyekuwa mtoto wa tatu wa Spika wa kwanza mweusi nchini,
Adam Sapi Mkwawa, alikuwa akifanyakazi katika kiwanda cha maji Afrika
cha Kidamali, Iringa.
Amewahi pia kufanyakazi katika Chama cha Wazalishaji Tumbaku Iringa na Shirika la Elimu Supplies.
Alizaliwa
Mei 4, 1949 katika kijiji cha Kalenga na kupata elimu ya msingi katika
shule za Kalenga na Tosamaganga kati ya mwaka 1956 na 1963.
Mwaka
1964 hadi 1970 alijiunga na shule ya sekondari Iyunga na Mkwawa, ambako
alipata elimu ya kawaida na ya juu ya sekondari kabla ya kujiunga na
elimu ya juu ya biashara na utawala 1971 hadi 1973.
Mmoja
wa ndugu wa marehemu, Hussein Sapi alisema mpaka umauti unamkuta, Abdul
Sapi Mkwawa alikuwa mtwa (chifu); alisimikwa mwaka 1999 baada ya kifo
cha baba yake, Adam Sapi Mkwawa aliyefariki Juni 25, 1999.
Kabla
ya maziko ya Chifu huyo, wazee wa kabila la Wahehe walimsimika Adam
ambaye ni mtoto wake wa tano kuwa chifu mpya wa kabila hilo.
Hata
hivyo, mtoto huyo anayesoma katika shule ya msingi ya Highlands ya
mjini Iringa, atalazimika kusubiri kufanya shughuli za kichifu mpaka
atakapotimiza umri wa miaka 20.
Tangazo
lililotolewa mbele ya Rais na ndugu wa karibu wa familia hiyo, Joseph
Mungai, ilisema mdogo wa marehemu, Saleh atashikilia wadhifa huo mpaka
mtoto huyo atakapofikisha umri huo.
Baada ya maziko , Rais Kikwete na msafara wake walizungumza na familia ya marehemu kijijini hapo.
0 comments:
Post a Comment