MWENDESHA PIKIPIKI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KISHA KUPORWA PIKIPIKI YAKE.
Mtu
mmoja mikocheni wilayani Mvomero mkoani Morogoro ameuawa kwa kupigwa
risasi shingoni na kisha kuporwa pikipiki aina Boxer ambapo jeshi la
polisi linawashikilia watu watatu waliohusika na tukio hilo.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amesema jeshi la polisi
lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuwakamata watu watatu
wanasadikiwa kujihusisha na tukio hilo na linaendelea kuwahoji kisha
watafikishwa mahakamani.
Aidha
kamanda Paulo amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa
aliye kimbia ambapo katika hatua nyingine wamefanikiwa kumkamata hawara
wa mtu huyo aliyejulikana kwa majina ya Husuna Isimaeli mkazi wa mkindo
ambaye alikuwa akimhifadhi mtuhumiwa na jeshi la polisi litaendelea
kumshikilia kwa mahojiano ilikumpata mtuhumiwa aliye kimbia.
0 comments:
Post a Comment