BREAKING NEWS..!! KAPTENI JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA.
Habari
zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kwamba Mbunge wa Mbinga
Magharibi (CCM), Kapteni mstaafu John Damian Komba amefariki dunia.
Kwa
mujibu wa vyanzo vya habari, Kapteni Komba amefariki katika Hospitali
ya TMJ, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi
ya sukari yaliyokuwa yakimsumbua.
Komba
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) atakumbukwa sana
kwa umahiri wa utunzi wa nyimbo mbalimbali za kwaya akiwa na TOT.
Miaka
mitatu iliyopita, Komba alipelekwa nchini India alikokwenda kufanyiwa
upasuaji kwenye nyonga, tatizo lililomsumbua kwa muda mrefu likichagizwa
na ule unene aliokuwa nao.
Upasuaji
huo ulilazimika kufanyika kwenye Hospitali ya Apollo kutokana na
Hospitali ya Muhimbili kuathiriwa na mgomo wa madaktari wakati huo.
Alipofika
India, madaktari walisita kumfanyia upasuaji kutokana na kuwa na mwili
mkubwa hivyo wakamwambia kuwa asilimia za kuamka katika upasuaji huo ni
ndogo lakini Komba akawasisitiza wamfanyie tu.
Tangu
wakati huo, Komba alikuwa na kibarua kikubwa cha kupunguza uzito kwani
awali alikuwa na kilo 138, lakini akajitahidi kupunguza hadi kufikia
kilo 128 ambazo pia aliendelea kupunguza hadi kilo 100.
Mungu ailaze roho ya Marehemu John Komba mahali pema peponi, Amen.
Kwa taarifa zaidi endelea kuperuz
0 comments:
Post a Comment