INASIKITIKISHA SANA !!!!MTOTO ALBINO ALIYETEKWA AKUTWA AMEUAWA MSITUNI KWA KUKATWA MIGUU NA MIKONO HUKO GEITA.
Waziri mkuu Mizengo Pinda akilia kutokana na mauaji ya albino chini Tanzania-Picha kutoka maktaba.
Mwili
wa mtoto Yohana Bahati aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja ambaye ni
mlemavu wa ngozi maarufu kama Albino, alitekwa siku ya Jumapili February
15, 2015 amepatikana ameuawa katika eneo la Shilabela Mapinduzi
kilomita kadhaa kutoka nyumbani kwao kijiji cha Ilelema .
Polisi
wanaeleza kuwa waliukuta mwili huo katika msitu wa hifadhi wa
Biharamulo leo majira ya alfajiri akiwa amekatwa mikono na miguu yake.
Wakati
mwili wa mtoto Yohana ukipatikana ,mama wa mtoto huyo bi , Ester Jonas
mwenye umri wa miaka 30 bado hali ya afya yake ni tete na amelazwa
katika hospitali ya rufaa ya Bugando, Mwanza .
Madaktari
walimfanyia upasuaji mwanamke huyo aliyekuwa amekatwa kwa panga usoni
mwake na sehemu zingine za mwili majeraha ambayo aliyapata wakati
alipokuwa akijaribu kumuokoa mwanawe, Yohana kutoka mikononi mwa wauaji .
Dada zake Yohana Tabu bahati mwenye umri wa miaka mitatu bado yuko mikononi mwa uangalizi wa askari polisi.
Dada
yao mkubwa ambaye pia ni Albino Shida Bahati mwenye umri wa miaka kumi
na miwili amehamishwa kijijini hapo tangu tukio hilo litokee, na
anatunzwa na jamaa zake katika kijiji jirani.
Mpaka
sasa watu wengine wawili zaidi wamekamatwa na polisi wakihusishwa na
tukio hilo ingawa baba mzazi wa mtoto huyo, bado anashikiliwa na polisi.
Mwezi
uliopita serikali ya Tanzania ilipiga marufuku waganga wa kienyeji pia
kupiga marufuku wapiga ramli wote ambao wanaelezwa kuchangia mauaji ya
watu hao wenye ulemavu wa ngozi.. waganga wa kienyeji wanaamini kwamba
viungo vya mwili wa Albino huleta bahati na utajiri kwa anaye
vipata.katazo hilo ni sehemu ya mkakati maalumu wa kupunguza
kama sio kuondosha kabisa mashambulizi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
0 comments:
Post a Comment