Ripoti
ya Taasisi ya Kuchunguza Makosa ya Ufisadi (SFO) ya Uingereza imewataja
mawaziri wawili wa serikali ya awamu ya nne kuwa walihusika katika
ufisadi wa zaidi ya bilioni 13.
Ufisadi
huo ulifanyika wakati serikali ya Tanzania ilipokopa Dola za Kimarekani
600 (shilingi trilioni 1.3) kupitia benki ya Standard ya Uingereza.
Baadhi
ya watumishi wa Benki ya Stanbic wametajwa kuhusika kuongeza asilimia
moja ya mkopo huo (kati ya shilingi bilioni 13 na 15)wakishirikiana na
waliokuwa watumishi wa serikali kati ya mwaka 2012 na 2013.
Ripoti
hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya Southwark Crown ya Afrika
Kusini, imewataja mawaziri wawili wa fedha wa zamani, Mustafa Mkulo na
Dk. William Mgimwa ambaye ni marehemu.
Mawaziri hao wanatajwa kuhusika kusaidia udanganyifu huo wakishirikiana na watumishi wengine wa umma.
Wengine
waliotajwa kwenye sakata hilo ni pamona na aliyekuwa Kamishna Mkuu wa
TRA, Harry Kitillya. Kwa upande wa Stanbic Bank tawi la Tanzania,
waliotajwa kuhusika ni Bashir Awale na Shose Sinare (Miss Tanzania
1996).
0 comments:
Post a Comment