Home » » Magufuli Kuyatumbua MAJIPU Yaliyojificha Ndani ya CCM.

Magufuli Kuyatumbua MAJIPU Yaliyojificha Ndani ya CCM.

Kasi ya Rais  John Magufuli ya kutumbua majipu serikalini inatarajiwa kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), mara tu atakapokabidhiwa rungu la uenyekiti na Mwenyekiti wa chama hicho kwa sasa, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.

Mara tu atakapokabidhiwa rungu la uenyekiti, Magufuli anatarajiwa kufanya kile kile anachoendelea kukifanya ndani ya serikali kwa kuwaumbua viongozi ndani ya chama hicho waliojigeuza miungu watu na wanaoharibu taswira ya chama.

Habari za ndani zinasema kuna viongozi ndani ya chama hicho ambao wamejimilikisha na wamekuwa wakineemeka na miradi mbalimbali ya chama hicho huku chama kikitegemea ruzuku ya serikali pekee kujiendesha.
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliandika jana katika ukurasa wake wa Twitter  kwamba baada ya kumaliza serikalini mabadiliko yatahamia kwenye chama.

“Tunachotaka kuwaambia wananchi ni kuwa baada ya kumaliza serikalini mabadiliko yatahamia kwenye  chama,” aliandika kwenye ukurasa wake
 
Mmoja wa viongozi wandamizi ndani ya CCM amedokeza kuwa  Magufuli anatarajia kutembeza fagio la chuma atakapokabidhiwa uenyekiti ili kurudisha heshima ya chama hicho kwa jamii.
 
Alisema hivi sasa wafanyabiashara wengi na matajiri wamekimbilia CCM na wengine kutumia mamilioni ya fedha kutafuta vyeo ikiwa ni ujanja ujanja wa kuficha maovu yao.

“Hivi sasa kama huna fedha usijisumbue kugombea nafasi ndani ya chama maana hutapata kitu, chama ni kama kimegeuka cha matajiri maskini hawana chao tena sasa Magufuli hatapenda kuona hali hii ikiendelea kuna watu lazima watakwenda na maji,” alisema kiongozi mmoja
 
“Imefikia wakati watu wenye tuhuma mbalimbali za ufisadi na wengine wakituhumiwa kwa kufadhili vikundi vya ujambazi wanawania kuteuliwa na chama kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama ….ndiyo maana wananchi wakakichoka chama sasa, Rais Magufuli kwenye kampeni zake za urais alibaini hilo na lazima atembeze fagio la chuma,” alisema kiongozi huyo.
 
 Imekuwa kawaida kwa Mwenyekiti wa CCM kumwachia nafasi hiyo Rais aliyeko madarakani hata kabla ya muda wa uchaguzi ndani ya chama hicho haujafika.

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Hassan Mwinyi, alimwachia, Benjamin  Mkapa nayeye Mkapa alimwachia, Jakaya Kikwete mwaka 2006.
 
Kama utaratibu huo utaendelea watu wengi wanatarajia, Mwenyekiti wa sasa wa CCM, Kikwete atamkabidhi nafasi ya uenyekiti John Magufuli mwakani.
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog