Home » » VIJANA WA BODABODA WAFANYA KUFURU MBEYA

VIJANA WA BODABODA WAFANYA KUFURU MBEYA




Mch Edward  mseve wa kanisa T.A.G ushirika wa uyole  amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na vijana ambao ni waendesha bodaboda  baada ya kuvuruga utaratibu wa ibada maalum ya mazishi katika kanisa hilo siku ya leo
Hayo yametokea baada ya kijana mmoja ambaye ni mwendesha bodaboda alifahamika kwa jina la Gabriel Ngalele kufariki dunia  na mch mseve kuanza ibada ya mazishi kanisani
Wakati ibada inaendelea vijana ambao ni waendesha bodaboda wapatao 300 walivamia kanisani hapo na kuchukua mwili wa marehemu huyo kwa nguvu na kuupeleka sehemu ya makaburini kwa ajiri ya  maziko 
Aidha vijana hao Wakiwa makaburini   waliendesha ibada   na hatimaye kuuzika mwili huo
Mch mseve ameeleza kuwa wengi wa vijana hao walikuwa walevi na wavuta bangi   kwani baada ya kuwatuliza vijana hao waache kupiga kelele wakiwa kanisani kwa ajiri ya maombi walianza kuhamaki na    kitu ambacho amedai kuwa huenda ndo kimechangia kuichukua maiti hiyo bila kufuata utaratibu
Mch huyo ameongeza kuwa hawezi kuchukua hatua zozote kwani hawajamdhulu kwa lolote huku akinabaisha kuwa hayo yote amemwachia mungu ashugulike na suala hilo
Hata hivyo kwa upande wake wa jeshi la polisi mkoani mbeya lilijaribu kutuliza kitendo hicho lakini lilishindwa kuwadhibiti vijana hao   kutokana na wingi wa mabodaboda  hao.

Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog