Home » »

BAADA YA KAZI NZITO 2013, KWETU PAZURI WAPONGEZANA

Sarah Uwera mmoja kati ya solo hodari wa Ambassadors akiwa katika pozi.
Baada ya kazi nzito ya utumishi waliyoifanya mwaka jana, kwaya ya mabalozi wa Yesu ama waite Ambassadors of Christ wanaofahamika zaidi kwa album yao ya Kwetu Pazuri kutoka nchini Rwanda, waliamua kuwa na siku ya kipekee kwa wanakwaya wote kwenda ufukweni kupongezana kwa kazi ya kumuhubiri Kristo wanayoifanya.

Katika pikiniki yao iliyofanyika ufukwe wa Rwesero huko nchini kwao, walishinda pamoja wakipeana shuhuda, kula pamoja, michezo pamoja na uimbaji ambapo uongozi wa kwaya hiyo uliwapa vyeti vya heshima baadhi ya wanakwaya wa kwaya hiyo kwa utumishi wao wa kumuhubiri Kristo kupitia kwaya hiyo. Ambapo pia kwaya hiyo ilitumia muda huo kutiana moyo wanakwaya wote tayari kwa kumtangaza Kristo kwa mwaka 2014


Twendeni mabalozi tukapunge upepo.
Mandhari saaafi.
Picha ya pamojaaa.

Sijajua haya matofali yanawekwa chiniii ama yanataka kurushwa mwe!
Facebook Blogger Plugin: Bloggerized by Joseph Kipangula Enhanced by Joseph Kipangula

0 comments:

Post a Comment

NURU FM 93.5 IRINGA

.

.

.

Nyali

Pages

Pages

Powered by Blogger.

Blog Archive

Search This Blog